Hatimaye yametimia kwani Rais wa Misri katimuliwa madarakani baada ya wananchi kufanya maandamano yasiyo na ukomo ikiwa ni miezi michache imepita tangu achaguliwe kama Rais wa Misri baada ya kuondolewa kwa Rais Mbaraka. Aidha Morsy amekuwa akishutumiwa tangu awali kwamba tangu aingie madarakani alikuwa akitengeneza mazingira ya kuwa mfalme na si Rais, walisikika wakilalamika baadhi ya wananchi.
