Msanii Baby Madaha Katika Pozi
KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu na muziki Baby Joseph Madaha amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuibiwa nguo zake za ndani alizokuwa ameanika nje maeneo ya Mikocheni jijini Dar. Baby Madaha “Alizifua kama dazeni nzima hivi na kuzianika nje kisha kwenda kwenye mishe zake. Heh! Kumbe vibaka hawaachi kitu, waliruka fensi wakazichukua pamoja na ndala.”
Katika kujua ukweli wa habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Baby Madaha na alipopatikana alisema ni kweli alilizwa nguo hizo na kudai anafanya jitihada za kuhama kwani eneo analoishi limezidi kwa wizi.
