Vunja Mbavu https://www.vunjambavu.com Kucheka Ni Dawa Sun, 16 May 2021 08:29:40 +0000 en-US hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.1.2 Vunja Mbavu Kucheka Ni Dawa false Washua Na Simu Janja https://www.vunjambavu.com/washua-na-simu-janja/ https://www.vunjambavu.com/washua-na-simu-janja/#respond Thu, 08 Sep 2016 23:35:55 +0000 http://www.vunjambavu.com/?p=5079 Washua Na Simu Janja

Simu Kiganjani

Wazee wengi ni watata na wanakuwa manunda sana wakiwa nyumbani. Sio rahisi sana kupiga stories na dingi kila wakati.

Lakini siku hizi muda pekee ambao unaweza kuzoeana na dingi ni pale unapomfundisha kutumia simu ya janja yaani simu za kupangusa.

Huwa wanakuwa wapole sana aisee yaani hapa unaweza hata kumwagiza maji ya kunywa na akakuletea huku umepiga nne kwenye kochi!

Chezea simu za kupangusa …………………….

 😀   😀   😀   😀   😀   😀   😀   😀

]]>
https://www.vunjambavu.com/washua-na-simu-janja/feed/ 0
Dingi Kafeli Vibaya! https://www.vunjambavu.com/dingi-kafeli-vibaya/ https://www.vunjambavu.com/dingi-kafeli-vibaya/#respond Sat, 19 Dec 2015 22:22:13 +0000 http://www.vunjambavu.com/?p=4155 baba-na-mwana

MTOTO : Baba kwani mimi nimetoka wapi?

BABA: Dah!! Mwanangu mbona unaniuliza swali gumu hivyo? Ene-Wei, hebu kaa hapo nikuhadithie. Mimi na Mama yako siku moja wakati anatoka kazini. Tulikutana Kituo cha  Basi , Mvua kubwa ikaanza kunyesha, ikalazimika tuchelewe saaana kupanda basi.Kwa sababu tulikuwa tumekaa pamoja, nilimwona ameloana sana na mvua na alikuwa akitetemeka baridi. Nilimwonea huruma nikamwachia Jaket langu hapo ndiyo tukaanza kuzoeana.Baada ya miezi mitatu tukaona ni vema tuoane!.Tukawaeleza wazazi wetu wakatukubalia, Harusi ikafanyika tena kubwa saana!! Tukaanza kuishi pamoja. Kwa kifupi ndiyo wewe ukapatikana. Ukikua kidogo utanielewa nina maana gani.

MTOTO: Haya, Ila Mwalimu atanipiga nisipomwambia kesho. Katuambia wote tuwaulize Wazazi wetu tumetoka wapi? Mwalimu wetu kasema yeye Ametoka TABORA !!!????

Akili za ngono bhana, Dingi kafeli!!.

]]>
https://www.vunjambavu.com/dingi-kafeli-vibaya/feed/ 0
Bobi Anayeongea https://www.vunjambavu.com/bobi-anayeongea/ https://www.vunjambavu.com/bobi-anayeongea/#respond Tue, 22 Sep 2015 22:12:44 +0000 http://www.vunjambavu.com/?p=3965 bobi

Bobi Anayeongea

Dogo mmoja alifanikiwa kuingia chuo kimojawapo nchini kwa mbwembwe sana. Katikati ya simesta, dogo akaishiwa hela na akaamua kumwandikia baba yake barua.

“Kwako baba,

Ni matumaini yangu hujambo. Huku chuoni mambo ni mazuri sana. Kuna maajabu hapa maprofesa hapa wamegundua njia ya kufundisha mbwa kuongea.  Mlete Bobi na shilingi laki 5, baada ya muda atakuwa anaweza kuongea.

Ni mwana’ko Dogo.”

Mzee wa watu haraka akatuma mkwanja na mbwa wake chuoni. Haikuchukua muda mkwanja ukaisha. Dogo akamtumia baba yake barua nyingine kuwa walimu wameboresha programu kwani sasa wanaweza kumfundisha mbwa kusoma.

Mzee wa watu akaongeze kimilioni bila hiyana. Mzee huyu aliyekuwa tayari anajisifu kijiji kizima akauza ng’ombe akatuma mkwanja.

Likizo ikafika Dogo akabaki anawaza anaenda kumwambia nini baba yake. Alipofika tu baba yake akamuulizia Bobi wake. Denti akamuita baba yake pembeni.

Dogo: Baba hili nitakalokwambia sitaki mama asikie?.

Baba:Vipi tena??

Dogo: Jumapili iliyopita tumeamka vizuri na Bobi, yeye kama kawaida yake akaenda kuchukua gazeti la Mzalendo na kukaa kwenye kiti na kuanza kusoma, ghafla wakati anasoma akaniita akanambia hivi, “baba yako bado anaendelea na kale kachangudoa ka pale mtaa wa pili?”Nilishtuka!

Baba: (Akaingilia kati) Ungemwua hapo hapo mbwa mshenzi huyu anataka kuniharibia mambo yangu!

Dogo: Baba na mimi lilinijia wazo ilo hilo sikumchelewesha nikamtwanga nyundo ya kichwa!

Baba: Safi sana safi sana, wewe jembe langu!

]]>
https://www.vunjambavu.com/bobi-anayeongea/feed/ 0