Vunja Mbavu https://www.vunjambavu.com Kucheka Ni Dawa Tue, 16 Jul 2013 12:40:15 +0000 en-US hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.1.2 Vunja Mbavu Kucheka Ni Dawa false Je, Kuna Haja Ya Tanzania Kutoa Majeshi Yake Kulinda Amani? https://www.vunjambavu.com/je-kuna-haja-ya-tanzania-kutoa-majeshi-yake-kulinda-amani/ https://www.vunjambavu.com/je-kuna-haja-ya-tanzania-kutoa-majeshi-yake-kulinda-amani/#respond Tue, 16 Jul 2013 12:40:15 +0000 http://www.vunjambavu.com/?p=1748 Darfur 1

Hawa ni baadhi ya askari wa Tanzania walijeruhiwa Darfur wakipata matibabu.

Kuna wakati unaweza ukajiuliza maswali, hivi ni kweli Tanzania tuhahitaji kuendelea kupigana vita ya nchi ambazo zimeshindwa kujitawala? Kwa manufaa ya nani? Na kwa nini nchi hizi zinaendelea kukosa utulivu? Inatuathiri nini iwapo tukaziacha nchi hizi? Je, kipato chetu kinatosha kushiriki vita za wenyewe kwa wenyewe?

Maswali haya na menngine mengi ni muhimu kujiuliza kwa sababu ya swali moja la msingi, ni nani anayefadhili makundi ya kiasi Afrika kwa kuyapa pesa na silaha? Hili swali ni muhimu kwa sababu mwisho wa siku sisi ndio tunaambiwa tukalinde amani katika nchi zenye waasi ambao hatujui ni nani anawafadhili. Kwa maswali haya ni dhahiri kwamba huu ni mchezo mchafu na kuna mkono wa mtu nyuma ya pazia!

Kwa mfano leo hii CHADEMA  wawe waasi kuipindua serikali ya CCM kwa mabavu halafu wakutwe wana silaha nzito za kivita; swali kubwa litakuwa wamezitoa wapi? Wamenunulia fedha kutoka wapi? Na wanaingia vitani kwa manufaa ya nani? Haya ndiyo maswali magumu ambayo siku zote viongozi wetu hutoa majibu mepesi, “wanaenda kulinda amani!”

Si vibaya kwa jirani kukiungua uende ukasaidie kuzima moto lakini kama jirani atakuwa anachoma nyumba yake makusudi ili ukamsaidie kuzima moto kila mara itafikia wakati azime mwenyewe na na akishindwa na aungue! Wala hii sio roho mbaya wakati mwingine watu hujifunza kwa njia zilizo ngumu! Mfano mzuri ni Rwanda, sitayazungumzia sana yale yaliyotokea Rwanda kwa sababu wengi mnayajua!


Hakikana nasema hakuna haja ya Tanzania kuendelea kupigana kwa ajili ya mataifa yaliyoshindwa kukaa pamoja kwa sababu kuu zifuatazo:-

  1. Hakuna asiyejua kama Tanzania imepigani nchi nyingi za Kiafrika zijipatie uhuru, kama ni mchango tumeshautoa sana kama Watanzania.
  2. je, ni kweli migogoro hii inayotokea katika nchi mbalimballi hususani Afrika imekosa utatuzi? Sidhani ninaamini kuna watu wapo kutengeneza migogoro kwa maslahi yao wanayoyajua wao, naamini watu wakipigana wengine watauza silaha!
  3. Mataifa makubwa yaliyoendelea kiuchumi ndio chachu ya migogoro mingi Afrika, hivyo kama ni kulinda amani mataifa hayo yatoe watu wake.
  4. Uchumi wa nchi yetu bado ni mdogo kutufanya kutumia jeshi katika vita isiyotuhusu, mtakumbuka vita ya Uganda ilivyotutia umasikini. Kupigana vita ni gharama kubwa sana ambayo hatuiwezi.
  5. Kumekuwa na uhalalishwaji wa wanaoitwa waasi kukubalika na mataifa makubwa, mfano mzuri ni Libya hivyo ni dhahiri kwamba watu wanapotoka kwenye mstari wa kiutawala kuna mataifa yanawaunga mkono na yawe ya kwanza kulinda amani.

Inawezekana kukawa na sababu nyingi zaidi za kuifanya Tanzania isishiriki katika vita hizi na zikatosheleza kurasa kadhaa za magazeti lakini ukweli unabakia pale pale, tunapigana vita isiyo na tija. Mawazo yangu nayaweza kuwa ya kiwendawazimu lakini ndio suluhu, aidha kuwaacha wamalizane ipo siku watapata akili kama Rwanda, au majeshi ya amani yawakamate waasi huko waliko, au nchi zinazotengeneza silaha ziache kuuza silaha kwa waasi!

 

]]>
https://www.vunjambavu.com/je-kuna-haja-ya-tanzania-kutoa-majeshi-yake-kulinda-amani/feed/ 0
CHADEMA Yaipiga Kumbo CCM Uchaguzi Wa Madiwani Arusha https://www.vunjambavu.com/chadema-yaipiga-kumbo-ccm-uchaguzi-wa-madiwani-arusha/ https://www.vunjambavu.com/chadema-yaipiga-kumbo-ccm-uchaguzi-wa-madiwani-arusha/#respond Sun, 14 Jul 2013 21:45:06 +0000 http://www.vunjambavu.com/?p=1727 Chama Cha  Demokrasia na Maendeleo (CDM) kimerejesha kata nne zilizokuwa zinagombaniwa katika uchaguzi mdogo mjini Arusha siku ya Jumapili na hivyo kuendeleza ubabe wake dhidi ya chama tawala katika mji huo ambao ni lango kuu la maeneo ya utalii nchini. Ushindi huo wa ngurumo umekuja baada ya waliokuwa wanachama na madiwani wa CDM kuvuliwa uanachama baada ya kufanya uasi na kusababisha viti vinne vya udiwani kuwa wazi kitu kilichosababisha kuitishwa kwa uchaguzi mdogo. Uchaguzi wa kata hizi nne umefanyika zikiwa zimepita karibu wiki kadhaa tangu kufanyika kwa chaguzi nyingine ndogo ambapo katika kata za Arusha uchaguzi wake uliahirishwa kufuatia mlipuko wa mabomu katika mkutano wa kampeni wa CDM ambapo watu watatu waliuawa na wengine zaidi ya sabini kujeruhiwa.

Matokeo Ya Uchaguzi Mdogo Wa Madiwani – Arusha

Na. KATA CHADEMA CCM CUF
1 Elerai 1715 1239 213
2 Kaloleni 1019 389 169
3 Kimandulu 2665 1169 –
4 Themi 678 326 313

 

Kimsingi, CDM imeshinda kwa zaidi ya asilimia 61 ya jumla ya kura halali zilizopigwa; ni ushindi wa radi! CCM wametumiwa ujumbe mzito wa kuwafanya watafakari kama wapo watu wenye kutafakari.

Kilichofanyika Arusha ni kichapo cha mwaka; ni uthibitisho kuwa kukataliwa kifikra hutangulia kukataliwa kivitendo na hapa vitendo ninamaanisha kura. Kwamba, kabla ya watu hawajabadilisha kura zao ni lazima wabadilishe fikra zao kwanza; wananchi wa Arusha walishabadilisha fikra zao kuhusu Chama cha Mapinduzi tangu 1995 walipomchagua Makongoro Nyerere wa NCCR-Mageuzi na toka wakati ule mahusiano yao na CCM hayajawa ya kawaida. Na siyo Arusha mjini tu ni katika Arusha ambapo tumeona upinzani ukizama hadi vijijini – Karatu, Mbulu, Arumeru Mashariki na Arusha Mjini kote ni wabunge wa upinzani na wote ni wa CDM. Ni mkoa wenye wabunge wengi wa CDM kuliko mkoa mwingine na mahali ambapo kama isingekuwa mizengwe basi Halmashauri karibu tatu za miji mbalimbali zingekuwa chini ya CDM.  Kwa matokeo haya na kama hakutakuwa na mizengwe ya CCM Meya ajaye wa Arusha atatoka CDM.

Wananchi wa Arusha hawakujali sana ahadi, vitisho, kejeli na vioja vya watawala; na ni wazi kabisa kuwa hawakujali zaidi milipuko ya mabomu na unyanyasaji uliopitiliza wa vyombo vya dola. Ni Arusha ambapo viongozi karibu wote wa CDM wamejikuta wakidhalilishwa, kufunguliwa mashtaka na kunyanyaswa na wale wenye madaraka ya kutawala. Kuanzia Mbowe hadi Slaa, Bi. Mushumbusi hadi Lema wote wamepata kibano chao mjini Arusha. Katika mazingira ya kawaida watu wanaweza kufikiria kuwa ili wawe “salama” na ili mambo yao yafanyike kwa “utulivu” si bora wachague CCM tu? Ni rahisi kabisa kuamini kuwa kwa kuchagua CCM Arusha ingekuwa imetulia na watu wake wana amani. Kwanini pamoja na ahadi hiyo ya nchi ya “maziwa na asali” wananchi wa Arusha bado wameikataa CCM?

Jibu linaweza kuwa ni gumu kidogo na lina mambo mengi. Kwa kuanzia tunaweza kusema kuwa wananchi wa Arusha wamekataa kupiga magoti mbele ya wanaowadhulumu na mbele ya watawala walioshindwa. Mwanadamu akinyanyasika sana kuna mahali anafika ambapo katika kukataa kwake kunyanyasika zaidi anaamua kukataa – kwa kiburi – kupiga magoti. Historia imejaa watu wa namna hiyo; watu ambao kwa kujitambua utu wao na thamani yao hawakuwa tayari kujisalimisha mbele ya watawala ili wapate amani ya uongo.

Lakini kubwa zaidi tunaweza kusema kuwa watu wa Arusha tofauti kulinganisha na mji kama wa Dar wengi wao ni wafanyabiashara na wanajitegemea wao wenyewe kwa maisha yao. Ni watu ambao wanashughuli mbalimbali ambazo hazitegemei ajira ya serikalini. Jiji kama la Dar kwa mfano lipo kundi kubwa sana la kipato cha kati ambalo linategemea maisha yake serikalini. Kundi hili kwa kiasi kikubwa ni kikwazo sana cha mabadiliko Jijini Dar kwani hawa ni watu ambao hata kama wanachukia yanayoendelea ni vigumu kuchagua upinzani kwa sababu hawaoni kama maslahi yao yatalindwa. Arusha na miji mingi ya pembezoni wako huru zaidi kuchagua bila ya kujali athari zozote kwenye ajira zao. Pamoja na kuchagua upinzani wananchi wa Arusha wameendelea kujipatia vipato vyao na ajira zao na utulivu ambao unatarajiwa kuja baada ya kuchagua chama wanachotaka kunaweza kurejesha amani na utulivu zaidi kama serikali na Chama cha Mapinduzi havitaendelea kuleta mizengwe.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huu yanatuma ujumbe mwingine zaidi. Kwamba, bado juhudi kubwa sana ya kukandamiza upigaji kura zinafanyika nchini na hili tumeanza kuliona tangu 2010. Katika hali ambayo haijawahi kutokea kabla ya 2010 upigaji kura ulikuwa chini ya asilimia 70 (asilimia karibu 40 hivi). Chaguzo zote kuu za nyuma yake upigaji kura ulikuwa kati ya asilimia 69 kwenda juu. Hata hivyo CCM ikitumia mbinu zinazoeleweka sana – vitisho, kukatisha tamaa, kufanya upinzani uonekane ni shetani, n.k imefanikiwa sana kukatisha tamaa ya kupiga kura hasa kwa wazee na kina mama. Hivyo, upinzani umekuwa ukitegemea kura za vijana zaidi kuliko za makundi mengine. Kundi hili la vijana sasa ndio ngome kuu ya upinzani nchini; na hawa ni vijana hasa ambao ama walipiga kura kwa mara ya kwanza 2010 au ndio wanapiga kura kwa mara ya kwanza sasa.

Lakini kuna kitu kingine ambacho naamini ni kweli zaidi kuliko hivi vingine na nilikidokeza katika posti yangu ya Facebook mapema leo; CCM inazidi kukataliwa na ahadi zake hazivutii tena kama zamani, vitisho vyake haviogopeshi na utukufu wake hautukuzwi tena. Ni wazi kabisa kuwa kukiwa na Tume huru, na mfumo mzuri wa uchaguzi CCM itapata shida sana kushinda na badala yake inahitaji sana kutegemea dola (polisi, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa n.k) kuweza kushinda. Hili ndilo tatizo kubwa sana; CCM ili kujirejeshea uhalali siyo tu ikubali kushindwa baada ya uchaguzi bali ichague njia yenye kuonesha kuwa uchaguzi ni huru na wahaki na hakuna njia nzuri ya kufanya hivyo kama kuhakikisha uhuru wa vyombo na uhuru wa sheria ya uchaguzi.

Hivyo, walichokifanya watu wa Arusha ni kuamua kuicharaza CCM kwenye sanduku la kura; kwani ni hapo tu ndipo sauti za raia zinaweza kusikika vizuri. Hofu ile ya kuwa CCM wataiba kura ni hofu ambayo imezuia watu wengi kupiga kura kwa sababu wanajiambia kuwa ‘CCM itashinda tu’ na matokeo yake hawaendi kupiga kura. Watu wa Arusha wamejua nguvu ya kura yao na wanajua sauti yao ni kura yao. Hawawezi kushindana na polisi na usalama wa taifa; hawawezi kushindana na Mkuu wa Mkoa na IGP; lakini wanajua sehemu pekee ambapo wana uwezo wa kushindana ni kwenye kupiga kura. Na hivyo wamejitokeza kupiga kura. Ni kama walipewa fimbo na kuambiwa waende wakawachape CCM na kuwachapa wamewachapa. Haikujalisha nani aliipigia kampeni CCM au jinsi gani CCM ilibebwa, mwisho wa siku (siku ya uchaguzi) uamuzi wa mwisho ni wa mtu mmoja mmoja; watu ambao walishafanya uamuzi wao kwenye fikra wakaenda kuuthibitisha kama kutia sahihi kwenye sanduku la kura.

Wananchi wetu wengi wakielewa nguvu hii kuu waliyonayo na nguvu ambayo inafanya demokrasia inoge watatambua kuwa iwe kwa mbinde au kwa upinde wataenda kupiga kura. Kwamba, haijalishi mabomu, polisi, kejeli au vitisho, ikifika wakati wa kupiga kura wataenda kupiga kura na kusema kile ambacho hawawezi kukisema kwa maneno.


CCM imekataliwa.  Na huu ni mwendelezo tu wa yale ambayo tumeyaona tangu 2010. Kazi kubwa ni kuwashawishi mamilioni ya wananchi wengine ambao kwa woga au kutokujua wanafikiri kuwa CCM inatakiwa kutawala milele.

Arusha wamesema hapana na wamerudia kusema hivyo tena na tena. CCM iheshimu uamuzi wa wananchi wa Arusha na iache mizengwe kwani haikisaidii chama kupendwa zaidi; CCM iangalie watu wake wanaoifanyia kampeni kama ni watu ambao wanastahili kuendelea na hilo kwani zaidi ya kuwafanya wapoteze kura, watu hao wamezidi kuifanya CCM ionekane ni kituko na kejeli na kudharaulika. CCM ikiendelea na watu wale wale na mbinu zile zile wapinzani hawana la kufanya isipokuwa kuendelea kucharaza watu bakora ya kura; ndio utamu wa demokrasia.

Hata hivyo yote ni sehemu ya demokrasia; Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye amesema vizuri kuelezea hili katika mtandao wa JamiiForums baada ya kipigo cha Arusha “Kuna watu wameuliza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa)”.

Shukrani: Mwanakijiji

]]>
https://www.vunjambavu.com/chadema-yaipiga-kumbo-ccm-uchaguzi-wa-madiwani-arusha/feed/ 0
Askari Saba Wa Tanzania Wadunguliwa Darfur | Walienda Kulinda Amani https://www.vunjambavu.com/askari-saba-wa-tanzania-wadunguliwa-darfur-walienda-kulinda-amani/ https://www.vunjambavu.com/askari-saba-wa-tanzania-wadunguliwa-darfur-walienda-kulinda-amani/#respond Sun, 14 Jul 2013 01:29:00 +0000 http://www.vunjambavu.com/?p=1697

kikwete-01

Wanajeshi saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa.Taarifa zilizotufikia jana zilisema kwamba wanajeshi hao wa Tanzania, wamekufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali.Kwa mujibu wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini.Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja.

Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo. Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.

Hii ni mara ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa wakivuka mto uliokuwa umefurika maji. Kanali Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogolea.

Tanzania ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.Wanajeshi hao wa Tanzania wametawanywa kwenye miji ya Khor Abeche na Muhajeria kusini mwa Darfur. Aprili mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana kuiangusha serikali ya DRC.


Majeshi ya Tanzania yalipelekwa kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa. Tanzania inaungana na nchi za Afrika Kusini na Malawi kukamilisha kikosi cha wanajeshi 3,000. Tanzania imepeleka wanajeshi 850. “Tanzania imekuwa ikijihusisha na misheni za amani, mafunzo na ushauri kwa nchi nyingi,” alinukuliwa Kanali Mgawe, na kueleza kuwa majeshi ya Tanzania yamekuweko katika vikosi vya kulinda amani huko Lebanon, Darfur, Sudan Kusini, Visiwa vya Comoro na Liberia. Liberia waliuawa wanajeshi wa Tanzania 11.“Tanzania daima haiendi kwa nchi yeyote bila ya kuombwa na nchi hiyo au kutoka Umoja wa Mataifa,” alisema. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mauaji hayo yaliyowakuta askari wa Tanzania.

Shukrani : Mwananchi

]]>
https://www.vunjambavu.com/askari-saba-wa-tanzania-wadunguliwa-darfur-walienda-kulinda-amani/feed/ 0
‘Masogange’ Adakwa Na ‘Unga’ Alikofia Ngwea https://www.vunjambavu.com/masogange-adakwa-na-unga-alikofia-ngwea/ https://www.vunjambavu.com/masogange-adakwa-na-unga-alikofia-ngwea/#respond Fri, 12 Jul 2013 12:04:13 +0000 http://www.vunjambavu.com/?p=1649 maso
HUKU skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi, Ijumaa linakupasha.

masogange
Agnes Gerald ‘Masogange’.

AWALI YA YOTE
Mwishoni mwa wiki iliyopita, habari ya mjini ilikuwa Masogange kanaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini. Habari zilisambaa kwamba sanjari na Masogange, mwingine aliyenaswa naye ni mdogo wake (mtoto wa mama yake mdogo Agnes) aitwaye Melisa Edward. Kwa mujibu wa habari hiyo ya mjini, wawili hao walinaswa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oriver Tambo uliopo Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania wakiwa na ‘mzigo’ wa kilo nyingi aina ya ‘crystal methamphetamine’ wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6.8!


MELISAEDWARD
Melisa Edward aliyekamatwa na Agnes.

IJUMAA LAANZA KUSAKA UKWELI
Baada ya kunasa habari hiyo, Ijumaa liliingia mzigoni kuusaka ukweli ambapo hata hivyo, madai hayo yalikuwa yakijifungafunga sana. Mtu mmoja wa karibu na Masogange alipoulizwa kuhusu ukweli au uongo wa habari hiyo alikuwa na haya ya kusema: “Ni kweli Agnes amekamatwa akiwa na madawa ya kulevya kule Sauzi. Lakini si yenye thamani hiyo ya bilioni sita bali ni milioni arobaini tu. Hata hivyo, ameachiwa kwa dhamana ila paspoti yake imezuiliwa. “Nadhani kuna mambo yanawekwa sawa ikiwezekana atarudi nyumbani.”

JIJINI DAR, KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ANENA
Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliviambia vyombo vya habari kuwa, Watanzania wawili walikamatwa nchini Afrika Kusini na mamlaka ya mapato wakiwa na madawa ya kulevya kutoka Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8. Kamanda Nzowa aliwataja Watanzania hao kuwa ni Agnes Gerald ambaye ana miaka 25 na Melisa Edward mwenye miaka 24. Alisema wawili hao baada ya kukamatwa na chombo hicho walikabidhiwa kwa polisi ambapo mahojiano yanaendelea.

IJUMAA LAMWIBUKIA KAMANDA NZOWA
Baada ya Kamanda Nzowa kuwataja kwa majina wawili hao Jumatatu iliyopita, siku iliyofuata, Ijumaa lilipiga hodi kwenye ofisi za kamanda huyo kwa lengo la kutaka kujua kama Agnes Gerald aliyemtaja jana yake ni Masogage au majina yanafanana tu. Kamanda huyo hakuwepo ofisini kwake asubuhi hiyo na kwa mujibu wa wasaidizi wake, alikuwa kwenye kikao cha dharura kwenye Ofisi za Polisi wa Kimataifa ‘Interpol’.

masogange1
Agnes Gerald ‘Masogange’.

APIGIWA SIMU
Ilibidi Ijumaa limsake kwa njia ya simu ya kiganjani kwa mara kadhaa. Alipopokea akaulizwa kuhusu Agnes Gerald aliyemtaja kama ni Masogange yule staa. Kamanda Nzowa: “Eee, mimi siwezi kusema ni huyo, ninachojua ni Agnes Gerald tu basi. Sasa kama ni Masogange mimi sifahamu lolote.”

UMANNE USIKU SIMU KUTOKA SAUZI
Mpaka hapo, timu nzima iliyokuwa ikifuatilia habari hiyo haikuona ukweli wa Agnes Gerald kuwa ni Masogange na kwa vile siku zote Global Publishers inasimamia utafiti kabla ya kuandika habari iliamua kuiweka pembeni kwanza ili kuendelea kuichimba. Saa 2:14 usiku wa siku hiyo, Ijumaa lilipokea simu yenye kuashiria wito (code number) ni ya nje na kabla haijapokelewa, ilibainika ni ya Afrika Kusini.


Ijumaa: Haloo.
Sauti: Haloo, mimi Masogange.
Ijumaa: Mambo Agnes, pole sana na mkasa uliokupata bwana, pole sana.
Agnes: Kwanza naumizwa sana na maneno ambayo watu wanazidi kuyaeneza sehemu mbalimbali bila kuwa na uhakika wowote, mimi sikukamatwa kwa sababu ya madawa ya kulevya.
“Mkasa nilioupata siyo ambao watu wanaueneza kwenye mitandao mbalimbali na katika vyombo ya habari.”
Ijumaa: Kwa hiyo madai ya kukutwa na madawa ya kulevya si ya kweli?
Agnes: Kweli nilikamatwa huku kwa matatizo f’lan ila siyo ishu ya madawa kama watu wanavyosambaza.
Ijumaa: Ni tatizo gani sasa?
Agnes: Unajua sipendi tena kuwapa watu faida ila lilikuwa ni tatizo la kawaida, nilikamatwa na baada ya hapo nilitoka na niko huru. Nasubiri tu kwenda mahakamani Ijumaa (leo) mara moja kisha n’tarudi Bongo.
Ijumaa: Mh! Sasa Egg, mbona huku mpaka viongozi wa polisi wamesema ni madawa?
Agnes: Hapana, siyo, ipo ishu ndogo tu.
Ijumaa: Haya pole sana kwa misukosuko.
Agnes: Asante sana, nitakuja huko siku si nyingi.
Habari hii imeandikwa na Imelda Mtema, Haruni Sanchawa na Musa Mateja.

]]>
https://www.vunjambavu.com/masogange-adakwa-na-unga-alikofia-ngwea/feed/ 0
GODBLESS LEMA AVAMIWA NA POLISI NYUMBANI KWAKE USIKU HUU! https://www.vunjambavu.com/godbless-lema-avamiwa-na-polisi-nyumbani-kwake-usiku-huu/ https://www.vunjambavu.com/godbless-lema-avamiwa-na-polisi-nyumbani-kwake-usiku-huu/#respond Thu, 20 Jun 2013 00:36:15 +0000 http://www.vunjambavu.com/?p=78 HABARI ZILIZOVUNJIKAVUNJIKA

lema

Habari zilizopatikana usiku huu zinaeleza kuwa mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema amevamiwa na polisi nyumbani kwake. Polisi wameruka ukuta na kuvamia nyumbani kwake majira ya saa sita usiku.

Taaarifa kutoka kwa mke wa Kamanda Lema kwa njia ya simu zinasema, polisi waliingia ndani kwa lengo la kumkamata Lema na kufanya upekuzi ambao haujawekwa bayana ni upekuzi wa nini! Saa 00:35 usiku huu ndio wakati walioondoka!

Endelea kuwa nasi tutakujuza zaidi kile kilichotokea!!!!!!!!!

**********


]]>
https://www.vunjambavu.com/godbless-lema-avamiwa-na-polisi-nyumbani-kwake-usiku-huu/feed/ 0