Waziri D.R.C. Atumbuliwa Baada Ya Kupiga Punyeto Ofisini

Punyeto

 

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amemfukuza kazi Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano baada ya kupiga punyeto akiwa ofisini.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Enock Ruberangabo Sebineza amefukwazwa kazi na Rais Kabila baada ya video yake akipiga punyeto kuenea sana kwenye mitandao ya kijamii.

Sibineza alifanya kitendo hicho akiwa ofisini kwake na Camera zilizokuwa zimefungwa ofisini humo kwa madhumuni ya ulinzi ndizo zilizomnasa.

Video yake yenye urefu wa dakika 4:27 inaonesha jinsi Naibu Waziri huyo alipoanza kitendo hicho akiwa ofisini kwake nyuma yake kukiwa na picha ya Rais wa Congo Joseph Kabila na bendera ya nchi hiyo. Watu wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na kitendo hicho wengine wakisema kuwa ni kiwango cha juu sana cha kashfa kwani ni aibu mtu mzima kama yeye kufanya kitendo kile.

Angalia Video Hii Kwa Hiyari Yako Mwenyewe

Comments

comments