well

Massawe alikuwa anafanya usafi wa kisima chake alichokichimba maeneo ya huko Kitunda alikojenga na anakoishi. Wakati anafanya huo usafi kwa bahati mbaya akadumbukia kisimani.

Massawe akapiga ukunga na mkewe akaja mbio kuangalia nini kilichotokea! Baada ya kuona mumewe kadumbukia kisimani aliamua kuja na kamba mpya ili amnusuru mumewe!

Alipomrushia ile kamba kisimani ili Massawe aikamate na kutoka, Massawe akamwuliza mkewe,


Massawe: Umenunua shilingi ngapi hii kamba?

Mke: Buku kwa Bwashe!

Massawe: Rudisha, kwa Kimaro anauza jero fanya haraka nitazama!

**********


Comments

comments