wife fight

Wanaume Wengine Wanapenda Ugomvi

Kuna wanaume wengine visilani balaa. Jamaa mmoja alikuwa anakitabia kimoja cha kuwa mkali sana kwa mkewe linapokuja suala la kuombwa hela wakati yeye hana. Ilikuwa ni ngumu sana kusema hana hela ikitokea hana na badala yake anazusha ugomvi na kuwa mkali kwa kila jambo.

Siku moja mkewe akaomba hela ya kusuka na kwa bahati mbaya jamaa alikuwa hana kitu. Kuua soooo.. ikabidi aanzishe kufoka foka kila akitoka kwenye mihangaiko yake. Ikawa kila siku akirudi nyumbani anatafuta vijisababu visivyo na msingi!

Siku hiyo mkewe  akajitahidi kuweka mazingira safi. Sebuleni pakafagiliwa kufutwa na kupangwa vizuri, Chumbani kila kitu safi, Watoto wameogeshwa wanang’aa, Mke kajipamba kama siku ya harusi.

Mume akaingia na akaangaza huku na huko kila kitu poa, Kukaa kwenye kochi tu mara akaanza kufoka….

Mume: Mama Dula, mama Dula x3

Mke: Labeika Mume wangu!

Mume: Liko wapi lile vumbi lilokuwa hapa kwenye coffee table??

Mke: Si nimelifuta mume wangu kwani kuna nini!!

Mume: Kuna namba ya simu muhimu sana nilikuwa nimeandika juu yake!!

Mke: Mmmmhh!! Baba Abdallah!!! Yote hii kisa hela ya kusuka niliyokuomba? Basi usinipe tena!!!

Mume: Umesemaje???

Comments

comments