Olduvai Gorge: Wakenya Mna Hila Ya Kwapa Kama Mke Mwenza

Olduvai Gorge

Kuna jambo ambalo limekuwa likinikera sana ambalo limekuwa likifanywa na Wakenya mara kwa mara. Kenya imekuwa na tabia moja mbaya sana ya kutangaza vivutio vya Tanzania kuwa vinapatikana Kenya. Hili jambo naanza kuamini sasa ni mikakati ya nchi na wala halitokei kwa bahati mbaya.

Wametangaza sana duniani kwamba vito vya madini ya Tanzanite vinapatikana kutoka Kenya. Hakuna asiyejua kwamba wamekuwa wakitangaza Mlima Kilimanjaro upo Kenya. Pia wamekuja na mpya pale binti mmoja akihutubia umoja wa Mataifa na kutangaza Olduvai Gorge iko Kenya  huku akijinasibu fuvu la mtu wa kale liko Kenya hivyo watu wote anawaona kama ni Wakenya.

Ahaaaa! Majirani mbona mnakuwa na visa kama wake wenza? Hebu oneni aibu kidogo basi. Na ndiyo maana Tanzania imekuwa ikujiuliza mara mbili kuingia kwenye shirikisho la Afrika mashariki kwa sababu Wakenya mna hila. Kweli Wakenya tena mna hila za wake wenza!

Haitoshi mmekuwa mkisema hata Diamond Platinumz anatoka Kenya, hili nalo limekaa vibaya. Kumbukumbu zinaonesha pia mliwahi kumwalika Mrisho Mpoto kwenye moja ya matamasha yenu ya Kiswahili na mkasema ajitambulishe kama Mkenya!

Naishukuru serikali ya Tanzania kwa kutokukaa kimya, hawa jamaa ni wapuuzi na wameanza kunikera sana. Haya yote inaonekana hawajayafanya kwa bahati mbaya ni mipango ya makusudi kabisa ya kutuhujumu Watanzania. Tutawaambia ukweli mjue kwamba mna hila na ni wa kuogopwa kama UKOMA.

Huko tunakoelekea iko siku mtasema Tanzania iko Kenya. Naombeni niwakumbushe kuwa, ugomvi wa Tanzania na Uganda ulitokana na upuuzi kama huu wa kutamani mali ya mwenzako. Hata Mungu anatuamrisha katika amri ya kumi, Usitamani mke wa jirani yako, wala mali yake, wala mjakazi wake, wala punda wake wala chochote alicho nacho. Acheni tamaa maana tamaa ni mbaya. Nawadedicate Wakenya wote na wimbo TAMAA NI MBAYA – 20 Percent. Mnakera sana majirani!

Kama Ni Mtanzania, Sambaza ujumbe Huu Kadri Uwezavyo

Comments

comments