Utajiri Ni Shida

salio

Jamaa mmoja alikosea kutuma pesa akatuma milioni mbili kwenye namba ambayo si kusudio lake. Akafikiria cha kufanya akaja na hii:

”Hello natumai u mzima. Naamini umepokea pesa niliyokutumia. Ni kwa ajili ya mwanzo wako wa kuingia katika Amri za Freemason kwa utambulisho mpya utakofanyika kesho saa 6 usku. Hiyo pesa ni kwa ajili ya nauli tu. Nitakutumia zaidi kwa ajili ya mavazi maalum. Sisi ni matajiri wa ufalme huu na tunakusubiri katika huu ufalme.

Yafuatayo ni mashrti, wiki mbili baada ya utambulisho mwanafamilia wa karibu zaidi na moyo wako atakufa, hii itafungua njia ya utajiri na utakuwa na uwezo wa kuruka usiku kwenda sehemu yoyote duniani.

Natanguliza shukrani. Lakini kama ikitokea haupo tayari kujiunga, tafadhali rudisha pesa la sivyo utakuwa shoga ndani ya saa 24 zijazo na baadaye utakufa siku tatu zijazo!”

Dakika tano baadae, jamaa akapata ujumbe unaosema;

“Tafadhali tuma milioni mbili zingine, rafiki yangu naye anahitaji !…..

Jamaa akazimia. Usicheke peke yako watumie na rafki zako!

???????

Comments

comments