Family-dinner

Msichana mmoja aliamua kumtambulisha mpenzi wake kwa wazazi wake. Aidha msichana huyo alikuwa hajawahi kufanya ngono na mpenzi wake na hiyo ilikuwa ni fursa yake kutoka na kulala na mpenzi wake kwa mara ya kwanza. Msichana huyo alimwambia ukweli mpenzi wake kwamba anataka Ijumaa ya siku hiyo watoke wote na watalala wote kwa mara ya kwanza ila kwa sharti la kukubali kuja kwa wazazi wake kwa ajili ya chakula cha usiku.

Yule mvulana akajua usiku wa siku hiyo ni lazima angelala kwa mara ya kwanza na mpenzi wake na kwa mara ya kwanza duniani. Hivyo aliamua kwenda duka la madawa kununua kondomu kwa ajili ya kujikinga.

Alipofika yule kijana alimweleza muuzaji ambaye ni Mfamasia kuwa alikuwa anataka kinga. Yule Mfamasia alimweleza kuwa kuna aina tatu za kinga ambazo ni 3 bomba, 10 bomba na family bomba.


Yule kijana alichagua family bomba kwani aliamini usiku wa siku hiyo angefanya kazi kubwa sana. Yule Mfamasia alimwelekeza kwa ufasaha kabisa namna ya kutumia kinga na akampa mafunzo yaliyodumu kwa takribani saa moja.

Saa ikawadia ya chakula cha usiku, yule kijana akaenda nyumbani kwa mpenzi wake wa kike na alipobisha hodi akapokelewa kwa furaha kubwa sana na mpenzi wake. Yule msichana alimkaribisha sebuleni ambako wazazi wake walikuwa wameketi tayari kwa chakula cha usiku. Kabla ya kuanza kula baba wa yule binti alimwomba mgeni aombee chakula.  Yule kijana akaanza kuomba na mara dakika 5, 10, 15 mpaka 20 yule kijana alikuwa bado anaombea chakula. Ikabidi yule binti amnong’oneze mpenzi wake ikiwa ni ishara ya kumtaka amalize kuomba.

Binti : Sikuwa najua kama wewe ni mlokole!

Kijana: Hata mimi sikuwa nafahamu kama baba yako ni mfamasia.

**********


Comments

comments