house-gal

Ni nadra sana kuona mfanyakazi wa ndani ‘house gel’ akidai kuongezewa mshahara mkubwa. Mara nyingi mahaouse gel wengi wakiona wanalipwa kidogo hutoroka bila mabosi wao kujua.

Lakini katika mitaa fulani ya Daslam, haouse gel mmoja alimweka kati mwajiri wake na kujikuta anaongezewa mshahara mara dufu kiulainiiiiiiiii! Mkasa huo ulikuwa kama ifuatavyo.


House gel: Bosi, nina shida!

Bosi: Shida gani?

House gel: Naomba uniongezee mshahara!

Bosi: Nipe sababu tatu kwa nini nikuongezee mshahara!

House gel: Mimi napika vizuri kuliko wewe?

Bosi: Nani amesema?

House gel: Baba (Akimaanisha mume wa huyo bosi).

Bosi: Sababu ya pili?

House gel: Mimi najua kunyoosha nguo kuliko wewe!

Bosi: Nani kakwambia?

House gel: Baba!!!

Bosi: Na sababu ya tatu? (Huku akianza kufura kwa hasira?)

House gel: Mimi nayajua majambozi kitandani kuliko wewe!

Bosi: (Kwa hasira) Mume wangu ndivyo alivyokwambia?

House gel: Hapana, kaniambia dereva. Kasema mimi ni mtamu kuliko wewe!

Bosi: Shii shii shiiiiii…! Usionge sana, nilikuwa nakupa elfu thelathini kwa mwezi badala yake nitakupa laki tatu! Usimwambie baba!

House gel: Asanteeeeeeeee!!!!!! (Huku anacheka)

**********


Comments

comments