family-safari

Mzee Macha wa Mbokomu Moshi Kilimanjaro leo asubuhi kaamka na kuchukua simu yake ya kiganjani kisha kampigia mwanae anayeishi Afrika Kusini.

Baada ya salamu akamwambia kijana wake, “nimechoka kuishi na mama yako na leo tunatengana rasmi.” Kijana akamwambia, “Mzee usifanye hivyo ngoja nimpigie Dada Wa Washington DC Marekani nimwambie.”

Dada alipopewa taarifa akahamaki na kumpigia Mzee na kumwambia, “naomba msifanye chochote, kaka na wengine wote tunakuja nyumbani. Tafadhali sana Baba usifanye chochote”, alisisitiza binti.

Baada ya kukata simu Mzee akamfuata mke wake akamwambia,  “chezea mimi wote wanakuja kula X-mass hapa nyumbani andaa mbege ya kutosha.”

Kweli hii ni time ya kuhesabiwa, akili kumkichwa!

Comments

comments