Tazama Ligi Ya Uingereza (EPL) Bureeeeeeeeeeeeeeeee!!!

gsky-2

Ligi ya Uingereza ni moja ya ligi za kabumbu ambazo zinaangaliwa na watu wengi sana duniani. Watu wengi wanapenda kuangalia mchezo wa soka. Lakini tatizo kubwa linalowakumba ni uwepo wa gharama kubwa sana za kumiliki na kulipia ving’amuzi ambavyo hurusha michezo hiyo.

Vipo vituo mbalimbali vya runinga vya kigeni hurusha michuano hiyo kwa gharama kubwa sana. Leo hii nitakupa njia ya uhakika ya kuangalia michuano ya ligi ya Uingereza pamoja na michuano ya Ulaya bure kabisa.

Napozungumzia bure nina maana zile gharama za malipo ya kila mwezi. Gharama hizi ndizo kubwa zaidi kuliko gharama za kununua vifaa vyake hata kwa vituo vya runinga vya kulipia. Yapo mambo ambayo utayagharamia mara moja tu kama ifuatavyo:

 • Receiver ya GSKY V3, V5, V6 au V7 (Nakushauri ukipata V6 au V7 ni bora zaidi)
 • Dish kubwa la futi 6 au sentimeta 120, ukipata zaidi ni bora zaidi
 • Fundi

Baada ya kuwa na vitu hivyo basi utaweza kuangalia soka nyumbani kwako bure kabisa.

gsky

GSKY ni nini?

Hii ni receiver ya kisasa kabisa ambayo huwa inafungua nambari za stesheni zote za runinga zilizofungwa kwa POWERVU.

Kwa nini GSKY?

Zipo receiver kadha wa kadha ambazo hufungua stesheni za POWERVU lakini GSKY hufungua bila kuweka nambari za kufungulia. Yenyewe huwa inajifungua ‘Automatic’. Hii ina maana huna haja ya kujua chochote zaidi ya kuwasha na kuangalia mechi zako.

Receivers zinazofungua kwa kuweka nambari ni Receivers za Strong. Hata hivyo zipo baadhi ambazo zinafanya vizuri lakini Tatizo lake, nambari za siri zikibadilishwa matangazo hukatika mpaka utakapoweka nambari nyingine.

Ni Toleo gani la GSKY lafaa zaidi?

Matoleo ya 6 na 7 yanafanya vizuri zaidi. Hii ni kutokana na kuongezewa baadhi ya huduma ambazo huwezi kuzipata kwa matoleo ya nyuma.

Gharama zake zipoje?

 1. Receiver = Tsh. 270,000/= tu kwa oda!!!
 2. Dish= Tsh. 120,000/= (Inategemea ubora wa hilo dish, bei inaweza kupanda au kupungua)
 3. Gharama za Fundi = Tsh. 50,000/=

Kama unaweza kufatisha maelekezo basi unaweza kufunga mwenyewe bila fundi. Iwapo utapata changamoto ya kufunga basi mafundi wetu watakufungia au fundi yeyote aliye karibu yako atakufungia dish lako.

Kwa nini gharama hizi ni nafuu sana?

Hizi gharama ni malipo ambayo utayalipa mara moja tu na baada ya hapo hutalipia tena. Ukichukua jumla yake ukagawanya kwa miezi 12 utakuta kwa wastani unalipa Tsh. 37,000/= kila mwezi. Na hizi gharama utazilipa kwa mwaka mmoja tu baada ya hapo hulipi tena maisha yako yote.

Ni vituo gani unaweza kuviona kupitia GSKY?

Vipo vituo vingi sana lakini kwa leo nitaelezea uelekeo ambao unaweza kuona ligi ya Uingereza pekee:

Jina la setelaiti ni NSS 12 ipo nyuzi 57.0 E (Mashariki)
Frequency: 4132 R
S/R: 11250
LNB : CBand

Vituo vya Runinga:

 • MTV Worldwide TV – Matukio Maalum Live (Michezo Ya Aina Zote NBA, Tennis, EPL, UEFA etc.)
 • MSNBC-Habari USA
 • Fox News –Habari USA
 • CNBC – Habari USA
 • Sky News International – Habari UK
 • BBC World News – Habari UK
 • Sky Sports News HQ UK – Habari za Michezo UK
 • Sport 24 HD – EPL & UEFA Live ( Mechi Zote Kubwa Live na Marudio Yake)
 • Prime US – Filamu USA
 • ITV Choice – Filamu UK & USA
 • RTL International – Habari Urusi
 • Colors – Filamu India

Pia zipo stesheni nyingine nyingi kama VOA, Ethiopia TV na nyingine nyingi bure kabisa. Kwa ushauri na maswali wasiliana nami kupitia baruapepe yangu au Whatsapp. Au unaweza kuandika maoni yako chini ya maelezo haya.

Baruapepe: info@vunjambavu.com
Whatsapp: 0713 255 350

Comments

comments