Semina Songea

semina songea

Jamaa alimwaga mkewe kwamba anaenda Songea kwa ajili ya semina ya siku saba. Kumbe alihamia kwa mchepuko wake nyumba ya jirani.

Alipoamka siku ya kwanza, aliamua kuchungulia hali inayoendelea nyumbani kwake kwa sababu haikuwa mbali sana na pale alipokuwa amesafiria!

Ghafla alitahayari kumwona jamaa mmoja anayoka nyumbani kwake kavaa taulo lake huku anapiga mswaki.

Uzalendo ukamshinda akambwatukia jamaa huku akimwuliza, “wewe ni nani?” Jamaa akajibu, “mambo ya mjini haya jamaa yangu. Mume wa huyu demu kasafiri kaenda Songea, najivinjari kiaina hapa.”

Kwa uchungu yule mume aliyesafiri kwenda Songea akajibu kwa uchungu, “mshenzi mkubwa, ngoja nirudi kutoka Songea nakuua.”

😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀

Comments

comments