Salome Ya Diamond na Rayvanny Ni Hatari Tupu

salome ya Diamond

Wimbo wa Malaika ni moja ya nyimbo ambazo zimeimbwa mara nyingi sana na wasanii tofauti duniani. Hii ni kutokana na kuukubali wimbo kwa kuwa na mahadhi na ujumbe mzuri sana.

Ni jambo linaloumiza sana kuona Saida Karoli akiwa vile alivyo sasa wakati nyimbo zake zina nguvu kubwa sana na zinaishi. Saida aliimba nyimbo ambazo ni hatari sana. Ni moja ya wasanii wachache sana ambao wameimba nyimbo ambazo zinaishi.

Simba aka Diamond Platinumz amedhihirisha hilo baada ya kupakua kichupa kimpya hatari tupu. Wimbo huu wa Salome kashirikiana na Rayvanny (Simjui sana) lakini kaimba vizuri sana.

Ni toleo la aina yake kwa kweli ambalo linatukumbusha uwezo wa hatari na wa kutisha wa mwanadada Saida Karoli. Ubunifu walioongeza hawa vijana wanaufanya wimbo huu kuwa mtamu zaidi kuusikiliza.

Nafikiri popote alipo Saida anatabasamu kuona wimbo wake unaishi kwa namna nyingine tena. Wapo vijana wanaokimbilia kusema hii ni copy and paste! Diamond asingeweza kufanya hivyo bila makubaliano. Sikuwepo ila naamini haki miliki zimezingatiwa na jambo hili sio jipya.

Lady Jaydee aliimba Uzuri Sio Sura kwa toleo lake na pia Mr. Paul aliimba wimbo wa daraja la salender. Nyimbo ambazo ziliwahi kuvuma miaka ya nyuma.

Wimbo wenyewe huu hapa, soma uandishi wake:

[Ubeti 1: RayVanny]

Kioo hakidanganyi mama
Umejipodoa umepodoka
Mwendo na shape vyote mwanana
Mi suruali yanidondoka
Tukimbizane nini Salome wangu?
Hiyo michezo ya jogoo
Mbona watizama chini Salome wangu?
Ukimuona jongoo
Inama kidogo
Shika magoti
Mi nimesimama kama ngongoti
Mtoto jojo sio roboti
Chumbani bingiribingiri ‘samasoti’

[Kibwagizo: Diamond Platnumz]

Unantenkenyaga ukinyonga Salome
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Unantenkenyaga ukinyonga kweli
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Aaah orera bakuru vani
Orera ngambee
Orera na Zari ma
Orera ngambe

[Ubeti 2: Diamond Platnumz]

Utamu kolea a porokoto
Ting’ali ting’ali ndani kwa moto
Ntamnyongea msokoto
Nteme sumu kali kama koboko
Eeh mapenzi yananipa shida
(Shida mama)
Ni donda lisilokuwa na tiba
(Tiba bwana)
Usije baby ukanicharanga
Ukanichambua moyo kama karanga
Mie baby kwenye msambwanda
Huwa siendagi nge nge ni nga nga nga

[Kibwagizo: Diamond Platnumz]

Unantenkenyaga ukinyonga Salome
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Unantenkenyaga ukinyonga kweli
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Aah orera bakuru vani
Orera ngambee
Orera na Zari ma
Orera ngambe

[Ubeti 3: RayVanny]

Miee mwenzako nyang’anyang’a
Miee binzari we ndio nyanya
Baby kwang’waru
Nisimamie kama kangaroo
Ibane kangwaru
Babu Juma mpige kwakwaru
(Kwakwarukwa)

[Daraja]
Asa chambua kama karanga sasa
(Chambua kama karanga)
Ichambue kama karanga Salome
(Chambua kama karanga)
Asa washa, washa, moto washa, washa
Songa, songa, ugali songa, songa
Mpaka chini ka chi
Mpaka chini ka chi

Wenye wivu wajinyonge leo
(Wenye wivu wajinyonge)
Aaah wenye wivu wajinyonge sana
(Wenye wivu wajinyonge)
Wenye wivu wajinyonge kweli
(Wenye wivu wajinyonge)
Oooh wenye wivu wajinyonge sana
(Wenye wivu wajinyonge)
[Outro]

Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(Macho kodo!)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(Wale kodo!)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(Ukinyonga)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(We ukisonga)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa

*****

Nisikuchoshe sana, angalia hii video.


 

Hata hivyo video hii ya Diamond imenifanya niutafute wimbo wa Saida Karoli aliouimba muongo mmoja uliopita. Maria Salome pengine ndio jina la wimbo ambao ulibeba sana umaarufu.

Huu Ni Wimbo Wa Saida Karoli


 

Comments

comments