Sababu Sita (6) Kwa Nini King’amuzi Cha GSKY Ni Bora Zaidi Kwa Powervu

gsky-2

Makala hii inaweza kuleta mijadala na maswali mengi sana kwa wasomaji. Hata hivyo napenda kutumia fursa hii kuwafahamisha ni king’amuzi gani cha Powervu kinachofanya vizuri zaidi. Kama unatumia hiki king’amuzi au ukikijaribu basi utakubaliana nami kwa kile nitakachokueleza.

Vipo ving’amuzi vingi ambavyo unaweza kuangalia vituo vya kulipia pasipo malipo kama QSat, Tiger, FreeSat na vingine unavyovifahamu. Licha wa baadhi yake kufungu channels za runinga nguli sana duniani lakini bado GSKY imekuwa ni bora zaidi.

Nachoweza kusema hawa jamaa wengine hawako serious na ndio maana kuna baadhi ya channels hazifunguki kabisa. Kama unatumia GSKY basi una uwezo wa kufungua channels nyingi sana za Powervu. Kama hujui Powervu ni nini basi kuna siku nitaliongelea hilo pia.

Kwa ufupi Powervu ni mfumo wa kulinda channels ili zisiangaliwe bila malipo (Free To Air) wakati channels hizo ni za kulipiwa. Sasa kama unataka kuangalia lazima ulipie katika kampuni inayozirusha na utaona hizo channels.

Kwa sasa kuna ving’amuzi kama sita hivi vyenye uwezo wa kufungua channels zinazolindwa na mfumo wa Powervu. Japokuwa vipo vinavyofungua kwa kuweka nambari za ufunguo, vingine nusu yake hujifungua na nusu mpaka uweke nambari za funguo na vya mwisho ni vile ambavyo hujifungua vyenyewe bila kuweka nambari za funguo. Alpha box, Strong SRT, GSKY, GSHD, AONE, Azplay na Qsat ni ving’amuzi maarufu sana kwa kazi hiyo. Lakini mpaka sasa GSKY imethibitisha ubora zaidi kuliko vyote. Hizi ndizo sababu zake:

1. Servers na Coverage Bora Zaidi

GSKY ina servers na coverage nzuri sana kwani king’amuzi hiki huonekana karibia dunia nzima. Ukitumia king’amuzi hiki  utasahau kabisa kama unaanglia bila malipo kwa sababu hakuna tofauti na wale wanaotumia ving’amuzi vya kulipia. Picha ni nzuri na zinaubora mkubwa.

2. Usaidizi/Msaada Kwa Wateja

Timu ya GSKY ina wataalamu makini sana ambao hutatua matatizo yote ya programu za GSKY mara moja. Programu yao ni makini na inauwezo wa kufungua channels zote za powervu bila mtumiaji kujua kama zilibadilishwa. Wataalamu hubadili programu na kuweka mpya huku ile ya awali ikiwa bado inafanya kazi.

3. Waranti

Ving’amuzi vya GSKY huja na waranti ya mwaka mzima. Ukifuata masharti na vigezo vya waranti unaweza kuwarudishia king’amuzi na kikarekebishwa au kubadilishwa kabisa iwapo kitakuwa na matatizo. Hii ina maana wana uhakika na kazi yao.

4. Kujifungua Bila Kuweka Nambari za Funguo

Hii ndiyo sifa bora zaidi. Ving’amuzi vya GSKY hujifungua bila mtumiaji kujua kama channels zilifungwa. Kitendo hiki kinamfanya mtumiaji afaidi zaidi wala asiwe na mawazo ya kwamba nambari zinaweza badilika. Vipo ving’amuzi mechi ikianza wanabadili nambari na kuzipata unakuta mpaka saa moja imepita.

Ni mara moja tu katika kipindi cha miezi nane GSKY ilipata shida ya channels kutokuonekana na nilipopakua programu mpya nikaiweka kwenye king’amuzi kupitia flash channels zikarudi hewani kama kawaida. Nimekitumia kwa miaka miwili sasa na nilibadili software mara moja tu.

Uelekeo mmoja unaweza kuona EPL na UEFA kupitia MTN Worldwide na Sport 24 HD iwapo kuna mechi mbili zinaoneshwa kwa wakati mmoja. Na kwa kupitia uelekeo mwingine unaweza kuona Laliga na FA cup kupitia channels za Sony. Channels zote hujifungua zanyewe Automatic.

5. Muundo Bora

King’amuzi hiki ni kigumu na kimetengenezwa kwa bati gumu pamoja na plastiki jambo linaloongeza uimara. Huja na remote na wakati mwingine unaweza kukuta betri za remote pia.

6. Gharama

Changamoto pekee ya king’amuzi hiki ni gharama yake. Kutokana na ubora mkubwa kimekuwa na gharama ambayo si rafiki kwa watumiaji wengi.

GSKY wameamua kutengeneza toleo la 5 ambalo lina vitu vingi pungufu ukilinganisha na toleo la 6 na 7. Hii inapelekea bei yake kupoa kidogo. Toleo la 5 ni maalumu kwa ajili ya Powervu pekee. Nidyo maana bei yake imepoa kidogo.

Kuna toleo la 8 linakuja litakuwa na vikorombwezo vingi zaidi. Licha ya vikorombwezo hivyo bado channels zinazooneshwa kwa powervu zitaendelea kuoneshwa bure kabisa. Hii ina maana una uhakika wa kuangalia EPL, UEFA, FA na Laliga bure maisha yako yote!

Kama una maswali usisite kuuliza  hapo chini ili tucajili pamoja. Nipate watu watano ambao wako tayari kuwa mashahidi kwa wengine. Niwhatsapp sasa hivi kabla bei ya ofa hainaisha.

Bei Za Ving’amuzi

 • GSKY v6: Tsh. 250,000/=
 • GSKY v5: Tsh. 215,000/=

Mahitaji Mengine

 • Dish la futi 6 au 8
 • Kama uko mkoani pata Fundi wa Madish

Baruapepe: info@vunjambavu.com
Whatsapp: 0713 255 350

Angalia Video HiiTunaomba radhi kwa uoni hafifu, tumepunguza resolution ili file liwe dogo!
Oda ya King'amuzi
 • Jina*(Jina Kamili)
  0
 • Simu*(Nambari Ya Simu)
  1
 • Baruapepe*(Anwani Sahihi)
  2
 • King'amuzi*(Chagua King'amuzi)
  3
 • Ujumbe*(Andika Ujumbe Wako Hapa)
  4
 • 5

Comments

comments