Polisi Wa Marekani Wanatumia Ganja Nini? | Philando Castile

vita

Siku moja baada ya Alton Sterling kuuawa na polisi huko Marekani, Mwafrika mwingine amepigwa risasi nne zilizopelekea kifo chake. Philando Castile alipigwa risasi nne na afisa wa polisi aliyemtaka atoe kitambulisho na leseni yake.

Hata hivyo Philando Castile alitoa pia kibali cha umiliki halali wa silaha yake kitendo kilichompelekea yule afisa wa polisi kumfyatulia risasi Philando Castile. Akiwa katika gari lake, Philando Castile alikuwa kaambatana na mpenzi wake Lavish Reynolds wakiambatana na binti yao aliyekuwa kiti cha nyuma.

Philando Castile akiwa anaendesha gari katika moja ya barabara za Minnesota,Jumatano hii, afisa huyo alimsimamisha na Philando Castile aliegesha gari pembeni.

Baada ya shambulio hilo la kinyama, mwanadada Lavish Reynolds alipata ujasiri wa kurekodi tukio lile na kulirusha papo hapo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na kufanya kuwa tukio lililokuwa linashuhudiwa LIVE!

Hii Hapa Ni Video Yake

Comments

comments