Knock-out

Ujana umekuwa una mambo mengi sana. Huko Marekni katika jiji la Jersey, watoto watatu wanashikiliwa na polisi baada ya kudaiwa kuwapiga ngumi watu kadhaa barabarani na kusababisha kifo cha mmoja wao.


Wao wanauita mchezo wa mjini ambapo vijana hao huwavizia watu na kuwapiga ngumi maeneo ya shingo jambo ambalo huwapeleka chini bila kizuizi. Mchezo huu wanauita ONE HIT QUITTER yaani mhimiri pigo moja (Mtu anayestahimili pigo moja)! Pia wanauita Knock Out!

Kwao ni jambo la kufurahisha lakini kitendo hiki kimepelekea kifo cha mmoja wa watu waliopigwa na watoto hao. Angalia video yake kwa maelezo zaidi. Hizi ni picha za video zilizonaswa na kamera zilizopo mitaani kwaajili ya usalama.

Angalia Video


Comments

comments