Nyie Wanaume Mungu Anawaona

 makalio

Aisee nyie wanaume kweli mnawatesa sana wanawake. Hapo zamani mlikuwa mnapenda wembamba wenyewe mkawabatiza jina ‘English Figure’, wakawa wanajikondesha mpaka wanatia huruma.

Baadaye mkaanza kupenda sura nzuri hasa wanawake weupe. Kama kawaida yao kuwaridhisha wakawa wanajikoboa kwa mikorogo ya kisasa na ya kienyeji na kujikuta wanakuwa rangi mbili.

 

Sasa hivi wanaume mmekuja na staili mpya, hata mwanamke awe na pesa namna gani, awe mrembo kiasi gani, English au au bantu figure, mwisho wa siku mnaoa wanawake wenye makalio makubwa. Nao kama kawaida hawakutaka kuchelewa wakatumia fursa,wanabusti makalio kila uchao.

 

Yaani nawaza siku akitokea mganga aseme wanawake wenye makalio makubwa ni dawa ya utajiri au kupata ubunge. Sipati picha hapa mjini patakavyokuwa dili!

Ona Wengine Hawa Manavyowahangaisha

Sehemu Ya Kwanza

Sehemu Ya Pili

Comments

comments