Kumekuwako hulka ya watu kunywa sumu, kujipiga vitanzi au kujimwaga toka maghorofani na namna nyingine za kujiangamiza kwa sababu ya ‘ngono’! Inawezekana ikawa ni kauli kali na yenye kuumiza lakini huu ndio ukweli. Kama uliwahi kufikiria kujiua kwa sababu ya mapenzi ambayo mimi nayaita ‘ngono’ nitakuwa sikosei  kukuita mwendawazimu na ukae ukijua kwamba wewe ni mwendawazimu!


Kuna sababu nyingi sana za wewe kuwa mwendawazimu iwapo utaamua kujiua kwa sababu ya mwanamke au mwanaume unayeshiriki naye ngono akikuacha au kukutenda. Huna sababu ya kujiua kwa kuwa

  1. Hamjazaliwa wote na wala hukutarajia utakutana na mtu kama huyo duniani!
  2. Maisha ni matamu sana japo ni mafupi.
  3. Wala usiwe na papara ya kujiua kwa sababu hutaishi milele.
  4. Kuna watu wanaokujali zaidi ya huyo ambaye mlikutana baa, disko, msibani,kilabuni,uchochoroni,shuleni,chuoni au kwingineko popote ulikokutana naye ambao utawaumiza sana kwa sababu wanakupenda na unawahusu.

  5. Wanaume au wanawake wapo kibao duniani hapa wa bei poa mpaka aghali, haina maana dunia inakuwa imeisha kwako.
  6. Mapenzi ya dhati ni yale yasiyo ya kuumizana, akikuumiza ujue hana mapenzi na wewe!
  7. Ukijiua mwenzako ataendelea kula bata tu wala hana neno maana wewe ni mpumbavu!
  8. Haitakupa furaha wala ushindi kwa sababu utakuwa umekufa.
  9. Dunia nzima itakuona mpumbavu tu na hakuna atakayejali sana ukiachia wale wachache wanaokupenda yaani ndugu zako wa damu.
  10. Kujiua ni dhambi, kama kuna maisha baada ya kifo 100% hutayapata hayo maisha!

Je, bado una sababu za kujiua? kama unazo naomba ufunguke hapa chini!

Comments

comments