Naona Mwalimu Hunipendi

mwalimu

Alex ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Mtakuja. Siku moja mwalimu aliingia darasani na kuwataka wanafunzi wasome hadithi moja iliyokuwa inahusiana na wanyama.

Baada ya kuisoma ile hadithi kwa kina na kuona matukio ya ile hadithi, mwalimu aliamua kuuliza maswali. Swali hili lilielekezwa moja kwa moja kwa Alex.

Mwalimu: Alex! Simba akianza kukufukuza utafanya nini?

Alex: Nitapanda juu ya mti.

Mwalimu: Je, na simba naye akipanda juu ya mti utafanya nini?

Alex: Nitakimbilia mtoni niogelee.

Mwalimu: Je, simba naye akikufuata mtoni?

Alex: Mwalimu! (Huku kahamaki) Uko upande wangu au wa simba? Maana sikuelewi kabisa, kama hunipendi sema tu.

Comments

comments