ironsmith

Wakati mwingine unaweza kuzua ugomvi usio na mwamuzi! Mwanamke mmoja alitaka kumwonyesha mumewe ni namna gani bado analipa baada ya miaka kumi na tano (15) ya ndoa. Alifanya hivyo kwa kumtajia watu ambao wanahitaji kuwa naye kimapenzi.

Mke: Nina miaka arobaini na tano (45) lakini mmoja wa marafiki zako bado ananitamani na anaona ninalipa!

Mume: Ahaaaa! Atakua Kamau Saambovu huyo.

Mke: Haswaaaaaa! Umejuaje mume wangu?

Mume: Anajulikana huyo! Yeye ni mzee wa vyuma chakavu huyo!

Kilichotokea hapo hata sijui maana nilikuwa namwaga maji mtaroni nikarudi chumbani kwangu!

Comments

comments