Mwanafunzi Mtiifu

Mwalimu Majaliwa ni mwalimu pendwa katika shule ya upili ya Mtakuja. Wanafunzi wanampenda sana kwa sababu amekuwa akitoa nasaha nzuri sana kwa vijana wake.

Siku moja aliamua kuzungumuza na wanafunzi wake mara baada ya kumaliza kuwafundisha. Mwalimu alianza kwa kuuliza wanafunzi nini wanafanya baada ya school?

Mwanafunzi wa kwanza akajibu , “naenda kwa Fereji Kibwana kununua bangi.”

Wapili akajibu , “naenda kwa Fereji Kibwana kununua vidonge vya kulevya.”

Watatu akajibu, “naenda kwa Fereji Kibwana kununua bia.”

Wanne akajibu, mimi  huwa napumzika, nasoma Quran,navuta uradi na natafuta rizki.”

Mwalimu: Manshalah kijana mzuri na hodari sana. Na jina lako ni nani?
Mwanafunzi wa nne: FEREJI KIBWANA.

**********


Comments

comments