ndoa-hatarini

Siku ya tatu mvua imekolea Daslam wenye michepuko yao wakaamua kutumia mwanya huo ili kufanya yao! Mkasa mzima ulikuwa hivi:

Mume:  Halloo mke wangu.. yaani ni shidaa sitaweza kurudi nyumbani daraja limevunjika na kutoka morogoro kurudi Dar haiwezekani!

Mke: Mume wangu Morogoro ulienda bila kuniaga! ?


Mume: Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia!

Mke: Khaaa! Sasa watoto nani atawaangalia!!!

Mume: Unasemaje!??? Wewe uko wapi kwani???

Mke: Niko Bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi!

Mume: Unasemaje wewe mwanamke…????  Nakwambia hivi nikukute nyumbani ndani ya dakika 15!

Baada ya dakika 15 mume kafika nyumbani!!!!!!

Mke: Haya umefikaje kutoka Morogoro?


Mume:  Nilipewa lift na helikopta ya Rais nilikuwa na makamu wake pia!!!!

Mke: Wewe mwanaume si helikopta aliyokuwemo makamu wa Rais imepata ajali kabla ya kuruka uwanja wa ndege wa Dar es salaam..

Mume: Mimi ni majeruhi mmojawapo!!!!

Hahahahaaaaaa uongo mwingine bana…!!!!!!!!!!!!!!


Comments

comments