Mteja1

Sinema ilianza pale mvua iliyonyesha Dar es Salaam maeneo ya magomeni pale dada huyu alipoomba huduma ya kuvushwa kwenye dimbwi kubwa la maji.

Hakika mteja ni mfalme, wahenga walisema. Mafuriko yaliyoikumba Daslam jana baada ya mvua kubwa kunyesha yalizua kizumbumkuti pale mteja alipoamua kurusha ngumi kwa mtoa huduma wake!

Imekuwa ni kawaida kwa watu wengi jijini Daslam kutumia madhara kadha wa kadha ambayo huwa yanajitokeza kwa kujitengenezea pesa za chap chap!

Mteja2

Ghafla mteja akabwagwa kwenye dimbwi la maji!

Mteja3

Mteja akaamua kumshambulia mhudumu wake kwa makonde mara baada ya kumbwaga kwenye maji machafu.

Mteja5

Wasamalia wema wakaja kumwopoa dada huyo!

Mteja5

Masikini dada huyo alishindwa kuzuia kilio!


Comments

comments