mkuki

Siku moja mwanaume mmoja alifika kwake akiwa anahema akitokea kazini kabla ya muda wa kawaida. Akamwambia mke wake,

Mume: Jiandae haraka tuna safiri kwenda mbeya

Mke: Kuna nini??

Mume: Mama amefariki!

Mke: Mimi siwezi kwenda kilioni nikiwa hivi!

Basi mke akaenda saluni akaweka nywele vizuri na kubandika kope za macho. Aliporudi akaanza kupanga nguo,akamuuliza mumewe,

Mke: Huvo mama yako amefariki kwa nini?

Mume:  Mama yangu hana kitu, nimetoka kuongea naye sasa hivi.

Mke: Si umeniambia kuwa kuna msiba?

Mume: Ndiyo, mama yako  kafariki!

Ghafla mkewe akaanza kughalaghala na kupiga kelele,

Mke: Niwahishe haraka nyumbani nikamzike mama nisije kuta wamezika!

Mume: Siwezi kwenda msibani nikiwa hivi, subiri nikanyoe ndevu.

Ama kweli mkuki kwa nguruwe…!!!

Comments

comments