Jamaa alienda  kwa kinyozi na kamkuta kinyozi ana mnyoa mteja. Jamaa akamwuliza kinyozi  atamaliza saa ngapi kunyoa! Kinyozi akamwambia baada ya saa mbili atakuwa amemaliza kunyoa. Yule jamaa akaondoka zake na hakurudi tena siku hiyo!

Kesho yake, jamaa akarudi akamkuta tena kinyozi anamnyoa mteja, akamuuliza tena atamaliza saa ngapi! Kinyozi akamjibu atamaliza baada ya saa moja! Jamaa akaondoka kitendo hicho kilimshangaza sana kinyozi akaahidi  kumfutilia zaidi!


Kesho yake jamaa akaja tena akakuta kinyozi anamnyoa tena mteja kama kawaida na akauliza tena atachukua muda gani kumaliza kunyoa! Kinyozi akamjibu baada ya nusu saa! Jamaa akaondoka!

Kuona vile, kinyozi ikabidi atume mtu amfuatilie ajue kuwa anaenda wapi akitoka pale! Baada ya kumfuatilia mjumbe akarudi kwa kinyozi. Kinyozi akamwuliza mjumbe wake, “vipi umeona jamaa anakoenda?” Mjumbe  akajibu, “ndio nimemwona akiingia nyumbani kwako!” Kumbe jamaa alikuwa akitoka pale anaenda kwa mke wa kinyozi kuchakachua!


Comments

comments