Mjane Na Ujumbe Wa Simu

gumzo na mjane

MZEE moja alifika kijiji fulani akakuta mtandao wa simu unashika vizuri. Akaamua kumwandikia mke wake ujumbe mfupi wa maandishi aliyekuwa amemwacha mjini.

Bahati mbaya alikosea nambari akatuma kimakosa ule ujumbe kwa mtu mwingine ambaye ni mwanamke mjane aliyekuwa kapoteza mumewe siku za karibuni.

Mjane huyo alipokea ujumbe ili ausome maana bado watu walikuwa  wanamtumia ujumbe wa kumfariji kutokana na msiba. Aliposoma ujumbe palepale akazimia!!

Mwanaye alipoona vile akausoma ule ujumbe ambavyo ilivyoandikwa:

“MKE WANGU MPENZI NAJUA UTASHANGAA KUONA SMS YANGU KWAKO. KUMBE HATA HUKU NAKO MTANDAO UNAPATIKANA KAMA HUKO. NIMEFIKA SALAMA NAMATAYARISHO YA WEWE KUJA YAMEKAMILIKA HIVYO JIANDAE HAITOFIKA WIKI IJAYO NA WEWE UTAKUWA UMESHANIFWATA HUKU”

Mtoto naye palepale chaliiii, akazimia.

?????? Hata mimi nimezimia hapa

Comments

comments