mayai

Mayai Ya Kuku

Mama mmoja alikuwa anafanya usafi chumbani na ghafla kwa mara ya kwanza akakutana na kisanduku chini ya uvungu. Alipokifungua akakuta mayai 5 na shilingi milioni 1.Aliporudi mumewe akamuuliza,

Mke: Kisanduku hiki ni cha nini pamoja na haya mayai?

Mume: Kweli wataka kujua mke wangu?

Mke: Kwani siku hizi tunafichana!!

Mume: Tangu nimekuoa miaka mitano iliyopita nilijiwekea utaratibu kama nitatoka nje ya ndoa nanunua yai moja na kuliweka humu ndani ya kisanduku.

Mke: (Huku akifurahi)  Kumbe mume wangu umetoka nje ya ndoa mara 5 tu tangu tuoane miaka 5 iliyopita?Waliokuwa wanasema wewe mhuni ni wachonganishi tu. Na vipi kuhusu hizo milioni 1?!

Mume: Huwa nayauza mayai pindi yanapokuwa mengi na pesa naziweka humo!

Mke akadondoka chini na kuzimia….!

Comments

comments