ng'ombe

Kama unataka kupima ukuu na nguvu ya Mungu basi utangojea sana. Huko India katika mji wa Sirsi , jimbo la Karnataka kuna ng’ombe mmoja jike amekuwa akihuzunisha sana watu. Miaka minne iliyopita, kuna basi lilimgonga ndama, aliyekuwa mtoto wa ng’ombe huyo mwombolezaji.

Tangu mwaka huo, ng’ombe huyo hufika kila siku sehemu ambayo mwanaye aligongwa na hulisimamisha lile gari lililomgonga mwanaye kila anapoliona likipita.

Licha ya mmliki wa basi hilo kulibadili kwa kulipaka rangi tofauti na ile ya awali lakini bado ng’ombe huyo hulitambua na kulizuia kila siku alionapo likipita katika eneo ambalo mwanaye aligongwa.

Angalia Video Hii

Comments

comments