maxresdefault (2) NDOA BANA…..

Jamaa mmoja mfugaji wa ng’ombe alikuwa kwenye zizi la ng’ombe wake na daktari wa mifungo aliyekuwa anamsaidia namna ya kupandishe jike lake ili litunge mimba. Mkewe alikuwepo pia akawa anashangaa jinsi lile duma linavyompanda jike.

Mwanamke yule uzalendo ukamshinda akaamua kumtupia swali Dkt. wa mifugo.

Mke: Hivi hili dume hupanda mara ngapi kwa siku?

Daktari:  Kwa wastani mara sita kwa siku!

Mke: (Mke akamgeukia mumewe na kumwambia,) Unaona mume wangu! ….”

Mume akajifanya hajasikia lolote kwani alijua huu ushakuwa msala, lakini naye akajitutumua na kumwuliza daktari,

Mume: Hivi hizo mara sita kwa siku huyu dume huwa analipanda jike hilo hilo?

Daktari: Hapana, huwa anapanda majike tofauti!

Mume: (Mume akamgeukia mkewe huku akitabasamu,) Unaonaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!

Kilichoendelea hata sijui maana nilikuwa nimekuja kuchukua maziwa na nilivyopewa tu nikasepa zangu masikani.

Comments

comments