Mapenzi Ni Matamu Ila Acha Kiherehere!

mapenzi-matamu

Ama hakika mapenzi ni matamu sana ukimpata akupendaye mkashibana. Kumjali mpenzi wako ni jambo la msingi sana lakini ni vizuri kuepuka kuwa na kiherehe sana. Jamaa mmoja alijikuta taabani mara baada ya kumkurupukia mpenzi wake.

Jamaa mmoja alikuwa na demu wake ambaye alikuwa anamjali sana kwa kila kitu. Yule demu alikuwa kila anachotaka jamaa anatoa. Kwa ufupi jmaa alikuwa anamjali sana demu wake.

Siku moja kama kawaida jamaa aliamka asubuhi na kuchukua simu yake kisha akampigia mpenzi wake wa moyo.

Jamaa: Mambo baby umeamkaje?
Demu: Siko poa sana…
Jamaa: Nini mbaya mpenzi?
Demu: Nina mimba halafu sikupanga iwe sasa!
Jamaa: Khaaa! Mbona tulikuwa tunatumia kinga umepataje?
Demu: Kani nani kasema ya kwako?

Hivi navyooongea jamaa kakimbizwa Muhimbili kazimia kwa mshtuko! Kweli mapenzi ni matamu! Ungekuwa wewe ungefanyaje aisee?

Comments

comments