Mwanasheria-Mhaya

Haya ndio manjonjo ya Kihaya!Baada ya kumaliza degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya kuhudumia clients (wateja) . Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake, alimuona kijana mtanashati anakuja kuelekea ofisini kwake. Akajua ni mteja amemletea kesi. Ndipo akanyanyua mkono wa simu ya TTCL na kuanza kuongea, huku anajizungusha kwenye kiti cha kuzunguruka.


Wakati kijana alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yuko busy kuongea na simu ya muhimu.! Wakati anaongea na simu, alisikika akisema ‘

No no, no,… Absolutely no.!! Wajulishe hao lay persons wa New York kuwa siwezi kushughulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million.. Mimi ni proffesional Lawyer and im crossing the border to serve internaional community..

Akapose kidogo, akanywa maji.. kisha akaendelea,….

Naweza kuanza kukusanya primary evidece next week but tell them watume kwanza ten million kwa kuanzia….. hahahaah you dont know my account Mr.Rogers… Ok waambie watume kwenye akaunti ile ile waliyonitumia milioni 100 last month…

Akapose tena akameza fundo la mate na kurekebisha tai yake, kisha akaendelea….

..Okey, usisahau kumueleza mwendesha mashtaka mkuu wa Marekani (State Prosecutor) kuwa nitakuja New York mwezi ujao maana nitapitia kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu Mholanzi, kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niliyoagiza…


Wakati anaongea hayo yote yule kijana alikua ametulia tu anamuangalia bwana Rwegashora anavyojizungusha kwa madaha kwenye kiti chake huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu yaTTCL..

Baada ya kumaliza kuongea na simu, bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia yule kijana,

..Samahni sana, kwa kukupoezea muda wako, unajua tena hizi kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe…. Yani niko busy sana, ninapokea simu mpaka nimechoka. Na simu nyingi ni za wateja wa nje ya nchi.. Anyway nikusaide nini.?

Jamaaa akajibu,

Mimi ni mfanyakazi wa TTCL, nimekuja kuunganisha line yako ya simu, kwani haipo haweni tangu wiki iliyopita..

**********


Comments

comments