Baada ya stori nyingi za Prezida mpya wa Tanzania kutapakaa kila kona ya nyumba za watu, nchi, Afrika Mashariki, Afrika na duniani kote; mama mmoja aliona wivu sana na akawa anakasirishwa jinsi mumewe anavyomsifia sana rais huyo kuliko hata yeye mwenyewe (mkewe). Kuona hivyo yule mwanamke akaamua kupima bahari kwa miguu:

Mke: Mume wangu, siku hizi sikuelewi kabis!

Mume: Kwa nini mke wangu?

Mke: Taarifa ya habari ya saa mbili usiku unaisubiri tangia saa kumi jioni na hutaki tuongee chochote!

Mume: Nataka nijue Magufuli kaibukia wapi leo.

Mke: Sasa mimi na Magufuli nani mhimu?

Mume: Acha kumfananisha magufuli na vitu vya Kipuuzi mkewe wangu! Weee vipi!!!!

Comments

comments