taulo

Hakika kuna maduka mengine si ya kwenda kununua vitu unaweza kuumbuka. Dogo mmoja toka mkoani Singida alitua katika jiji la Daslamu! Baada ya tembea temba ya hapa na pale akaibukia Mlimani City. Huko alikutana na maduka mbalimbali yenye kuuza vitu vya kupendeza. Dogo ikabidi ajichanganye moja ya maduka hayo kupepesa macho na kwa bahati nzuri akanogewa na taulo la kuogea ikiwa ni mgeni jijini na alikuwa hana taulo.

Dogo: Taulo bei gani?

Muuzaji: Laki moja!

Dogo: Duh! Hili linafuta hadi dhambi nini?

Kilichoendelea sijui maana nilikuwa napita….

Comments

comments