Madenge

Madenge alikuwa mwanafunzi kilaza sana darasani. hakuweza kabisa kufaulu masomo yake hususani hisabati, kemia na fizikia. Alama zake zilikuwa 8 akijitahidi sana anapata 10.

Siku moja Madenge alifanya mtihani wa Hisabati. Mwalimu wao alikuwa na mazoea ya kuanza kugawa karatasi za mitihani kwa mwanafunzi aliye na alama ndogo zaidi kuelekea alama za juu.


Aliita majina ya wanafunzi huku akitaja alama zao kuanzia  8, 50, 60, 70 na hatimaye akafika 88. Alipokuwa anataja alama za juu watu walianza kugeuka kumwangalia Madenge kwani alikuwa hajaitwa!

Baada ya kutaja jina la mwanafunzi aliyekuwa kapata 88, mwalimu alibakiwa na karatasi moja na Madenge pekee ndiye aliyekuwa hajapata karatasi yake. Wanafunzi wakapigwa na butwaa na pia Madenge hakuamini kama amepata zaidi ya 88. Madenge akaanza kujikweza na kuweka pozi na mbwembwe kibao akiamini siku hiyo atawashangaza wengi kwa kufaulu somo la hisabati.

Baada ya hapo mwalimu aliendelea,

Mwalimu: Kuna hili jingine ndio zuzu la kutupwa, limepata sifuri na halijaandika jina lake. Nani hajapata karatasi?

Ungekuwa wewe ni Madenge ungefanyaje?

**********


Comments

comments