Maadhimisho Ya Kupatwa Kwa Jua

jua

Mkazi mmoja wa Rujewa ameushangaza umma pale alipomwomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ateue mkoa wa Mbeya kuadhimisha kupatwa kwa jua kwa mwaka mwingine tena. Akiongea na mwandishi wetu, mkazi huyo alisema kupatwa kwa jua kulikoadhimishwa mkoani Mbeya kumeleta wageni wengi na kuitambulisha sana Rujewa.

Aidha mwanahabari wetu alifanikiwa kuyanasa mazungumzo ya mkazi huyo wa Rujewa, mkoani Mbeya. Katika mazingira kama haya ni jambo la msingi sana kupeneyeza elimu kwa watu wote ili wajue tofauti ya maadhimisho na matukio ya asili.

Tunakoelekea maadhimisho ya kitaifa yatakuwa mengi sana kama hali hii haitadhibitiwa. Serikali ya hapa kazi tu ina kazi kweli msimu huu!

Sikiliza Hapa Chini

Comments

comments