Kuwa Zuzu Mzigo

zuzu

Jamaa mmoja alikuwa anatembea nyuma ya zuzu fulani. Mbele yao kulikuwa na noti ya shilingi elfu kumi chini. Mambo yalikuwa hivi:

ZUZU: Asante Mungu nimeokota elfu kumi!

JAMAA: Halo bro, hicho ulichookota ni kitambulisho changu tafadhari nakiomba.

ZUZU: Hata kama mimi chizi, ila si mjinga kiasi hicho! Hebu niambie jina lako nani?

JAMAA: Jina langu Benki Kuu Ya Tanzania.

ZUZU: Mh! Haya, una umri gani?

JAMAA: Umri wangu Ni Shilingi Elfu Kumi

ZUZU: Dah! Kweli aise, kumbe kitambulisho ni chako! Nisamehe kwa kutokuamini Braza!!!

Comments

comments