Kuna Wanaume Hawakuumbwa Kuoa

mume-na-mke

Zuzu alioa mke mzuri sana mpaka watu wakawa wanateta namna Zuzu alivyompata mrembo huyo. Mara baada ya miezi minne na nusu mke wa Zuzu akajifungua mtoto wa kiume. Zuzu akazusha kweli:
Mume: Nitakupa talaka uende kwenu. Utazaaje mtoto baada ya miezi minne na nusu. Kwani ni kuku wa kizungu!
Mke: Mswalie mtume mume wangu, hebu kaa chini tufanye hesabu.  Wewe tangu unioe ni miezi mingapi?
Mume: Minne na nusu tu!
Mke: Na mimi tangu niolewe ni miezi mingapi?
Mume: Minne na nusu!
Mke: Sasa “nne na nusu na nne na nusu”jumla ni miezi mingapi?
Mume: Loooooo sorry darling, wallahi nilikua nisha kudhania vibaya na talaka ilikuwa inakufuata.

?

Comments

comments