key

Siku moja binti mmoja aliamua kumwuliza babu yake maswali ambayo yalikuwa yanamwumiza sana kichwa. Jambo hili lilikuwa linamkosesha raha sana siku zote!

Mjukuu: Babu, mimi kuna jambo ambalo linanisumbua sana kichwani!

Babu: Lipi hilo mjukuu wangu?


Mjukuu: Hivi kwa nini mwanaume akiwa na wanawake wengi anasifiwa na kuonekana shujaa sana kwenye jamii lakini mwanamke akiwa na wanaume wengi anaonekana hafai na malaya?

Babu: Mjukuu wangu kuna jambo moja hulijui, funguo moja ikifungua makufuri mengi watu wataipenda sana hiyo funguo na wataiita ‘master key’ lakini kufuli likifunguliwa na kila ufunguo hakuna atakayelitaka kufuli la hivyo!

**********


Comments

comments