aseno

Unajua zile umepata demu wako halafu home huna Super Sport na hata kama unayo kuna raha yake kucheki mechi klabu ukiwa na washikaji! Kutokana na tatizo la kulalamikiwa na mpenzi wake kwamba anamwacha peke yake na anaenda kucheki mechi usiku, jamaa mmoja aliamua kutoka na demu wake kwenda kuangalia moja ya mechi kati ya Man U vs Asenane!

Mkasa mzima ulikuwa hivi;

Demu: Baby yule jamaa ni CHRIS BROWN?
Jamaa: Hapana anaitwa THEO WALCOT
Demu: Hee.. Ile kadi ya njano ni ya nini?
Jamaa: Ni onyo tu, akipewa nyekundu anatoka
Demu: Na ya kijani je?


Jamaa: Hamna kitu kama hicho
Demu: Nataka arsenal washinde KOMBE LA DUNIA
Jamaa: (kimya)
Demu: Yule mzee ni nani?
Jamaa: ARSENE WENGER
Demu: Ooky.. Kwaiyo na yule mwingine ni MANCHESTER WENGER..??”

Kwa maswali haya lazima jamaa alijutia kuja kuangalia mechi maana alitolewa kabisa mchezoni halafu ni demu wake kucheka anashindwa kumwelewesha anashindwa maana anaonyesha alikuwa anahitaji darasa la mwezi mzima!


Comments

comments