Kipunje-1

Kipunje akijiandaa kuingia uwannjani.

Madhani umeshawahi kuona soka la mchangani linavyoendeshwa. Huku mechi huwa zina ubabe mkubwa sana na mwamuzi anatakiwa awe mbabe vinginevyo ataishia kupata kichapo. Mechi za mchangani huwa mashabiki hawataki timu yao ifungwe na ikitokea mwamuzi ni sababu ya timu yao kufungwa basi mwamuzi huyo lazima awe katika wakati mgumu sana!


Kipunje2

Maandalizi yanaendelea.

Mwananyamala jijini Dar es Salaam nchini Tanzania anatokea mwamuzi anayevuta hisia zetu Vunjambavu na tukaamua kumtathimini. Jina lake ni Kipunje. Kipunje ndiye mwamuzi aghali zaidi kuliko kuliko waamuzi wote wa ligi za mchangani katika jiji la Dar es Salaam. Na ana umaarufu mkubwa sana miongoni mwa waamuzi wa ligi za mchangani. Hulipwa kati ya TZS 20,000/= mpaka 50,000/= wakati wengine hulipwa kati ya 10,000/= na 12,000/=

Kipunje6

Kipunje anaweka zana sawasawa.

Kivutio kikubwa cha Kipunje ni namna anavyojiandaa. Huvaa jezi zake yaani bukta na fulana za waamuzi, huchukua kadi zote za manjano na nyekundu, baada ya hapo Kipunje hujifunga kamba kiunoni na huweka panga kushoto kwake na shoka kulia mwa kiuno chake.

kipunje5

Ziko wapi kadi zangu!

Kipunje alianza kuingia uwanjani na silaha mara baada ya kumshuhudia mwamuzi mwenzake aliyefahamika kwa jina la Wema akiambulia kichapo mpaka akazimia.  Tukio hilo lilitokea mwaka 2005 wakati Mchangani FC ya Mwananyamala ilipofunga bao lililokataliwa na mashabiki wa Amstadam FC ya Tandale katika uwanja wa CCM Mwinyijuma jijini Dar es Salaam.

Kipunje3

Kazi sasa!

“Mwaka jana (2012) silaha hizi zilinisaidia sana. Pengine ningekuwa marehemu kwa sasa. Ilikuwa katika uwanja wa Mwinyijuma nilipokuwa nachezesha mechi ya nusu fainali kati ya Shideo na Bauda. Mashabiki wa Shideo waliingia uwanjani kwa lengo la kunipigakwa sababu tu nilikubali goli lililofungwa na Baula”, alieleza Kipunje.


“Hawakujua kama nina silaha, niliwaacha wanikaribie na wakaanza kunizongazonga. Ghafla nikachomoa upanga wangu lakini waliponiona natoa upanga wakashtuka na kutoka mbio”, aliongeza.

“Kwa bahati mbaya wakati nawakimbiza upanga ukadondoka na mmoja wao akauokota na kabla hajakaa sawa nilichomoa shoka langu alipoliona akatoka mbio na kuangusha upanga. Baada ya kuhakikisha wamefika mbali nilirudi uwanjani na kuendelea na kazi yangu”, Kipunje alibainisha.

“Si mashabiki tu, hata mateja wanaokusanyika uwanjani na wachezaji huwa wanajua kabisa nina silaha. Nikimwonyesha mchezaji kadi nyekundu huwa anatoka nje kwa roho safi kabisa”, alisisitiza.


Kipunje ana watoto watatu Zainabu (5), Zulfa (2) na Nasra (1) na anawake wawili wote anaishi nao nyumba moja huko Mwananyamala. Ana mpango wa kuchezesha ligi kuu baada ya kuhudhuria mafunzo ya TFF mwezi ujao. Chama cha soka cha Kinondoni kimekuwa kikimkataza asitumie silaha lakini alikataa kwa madai kwamba huo ni ulizi wake.

Mbali na kuwa mwamuzi, Kipunje piani utingo wa daladala inayofanya safari zake toka Makumbusho na Kivukoni. Jina lake kamili ni Issa Salum Mchinjakuku.

Shukrani: Sweetbert Lukonge

Chanzo: Mwanaspoti | 07-10-2013

**********

Comments

comments