Ibada na Wito

mchungaji-na-pesa

Ibada ilipokaribia kuisha Mchungaji alitoa wito kwa waumini wake, “anayetaka kuokoka anyoshe mkono.” Watu wote wakatulia kimya.

Tajiri mmoja akapita mbele akasema, “jamani Mchungaji anauliza anayetaka kuokoka anyoshe mkono.” Mtoto mmoja akanyosha, yule tajiri akampa mtoto laki tano papo hapo.

Tajiri akawageukia waumini akauliza tena “anayetaka kuokoka anyooshe mkono!” Waumini wote wakanyosha mikono juu. Lakini cha kushangaza, yule tajiri akageuka kumkabidhi mchungaji waongofu  akakuta Mchungaji naye kanyosha mkono. Chezea pesa wewe!!!!!!

Comments

comments