funeral

Baba mmoja alibahatika kuoa na kupata mtoto miezi kadhaa baada ya ndoa yake changa. Lakini baba huyo alikosa furaha mara baada ya kuhisi na kugundua kuwa yule mtoto hakuwa wake. Mara zote alikuwa akisemesha nafsi yake, “Huyu mtoto si wangu! Lazima nimwuee, aibu gani hii! Siwezi kulea mtoto ambaye si wangu!”


Yule baba akawa anatafuta namna ya kumwua kwa siri yule mtoto ili asimwumize mkewe. Baada ya mchakato wa kina katika kutafuta ufumbuzi hatimaye alipata njia mbadala ya kumwua yule mtoto. Njia hiyo pekee ilikuwa ni kuweka sumu kwenye matiti ya mkewe ili mtoto atakaponyonya anyonye pamoja na sumu ili afe.

Usiku wa manane, akamtegea mkewe akiwa amelala na kumpakaza sumu kwenye chuchu zake kisha akalala. Asubuhi kama kawaida yule baba akaondoaka kwenda kazini. Milango ya saa tano akapigiwa simu kwamba nyumbani kwake kuna msiba umetokea ghafla. Alipodadisi ni nani kafariki mtoa taarifa alisema arudi nyumbani kwanza taarifa zote atazipata huko.

Hivyo yule baba akatoka mbio mpaka nyumbani na kukuta watu wamejaa wanaomboleza msiba. Alipouliza nani kafariki akaambiwa house boy wake ndo kafariki ghafla. Unajua nini kilichotokea? Hebu jiongeze mwenyewe acha uzembe!

**********


Comments

comments