Kumekuwako tabia ya walio wengi kuweka taarifa zao muhimu katika ‘kitabu cha uso’ yaani facebook na kujaribu kuonyesha kila hatua ya maisha yao. Kiukweli dunia ina mengi na huwezi kujua nani anakuwazia nini na nani ni mbaya wako! Kama ilivyo kwa wengine ambao wanaweza kutongozana facebook, wakagusanisha vikojoleo vyao na maisha yakaendelea au wengine wanavyoweza kufanya biashara facebook na kutengeneza mabilioni; vivyo hivyo hata waharifu wanaweza kufanya uharifu kupitia facebook!

Sina hakika ni Watanzania wangapi wameathirika na uharifu wa facebook lakini nina imani wapo na pengine hawana tu pa kushuhudia. Binti mmoja wa Kispaniola aliweka picha yake nzuri facebook kama ilivyo kawaida ya wengi kuchagua picha nzuri na kuzitupia FB! Kwa hakika alipata maombi ya marafiki wengi sana na aliwakubali wote. Mwanaume mmoja alianza kumtaka kimapenzi inasemekana binti huyo alikataa lakini kwa sababu aliweka taarifa zake muhimu zote facebook ikiwa ni pamoja na anwani ya makazi, simu na nyinginezo ilikuwa ni rahisi kwa yuke mwanaume kumtafuta. Angalia video yake uone yaliyomkuta binti huyo!


Comments

comments