Elimu | Jifunze Namna Ya Kuvuna Filamu Katika Wavuti

pakua

Umewahi kufikiria ni namna gani unaweza kupakua filamu kutoka katika wavuti mbalimbali? Inawezekana ndio na inawezekana hilo jambo kwako ni gumu sana. Leo hii nitakupa njia rahisi ya kupata filamu kwenye wavuti ambazo zinaitwa ‘torrents’.

Hatua Za Kufuata:

1. Hakikisha una BANDO ya data ya kutosha, inafaa kwa wale wenye uwezo wa kuwa na internet bila kikomo.

2. Pakua programu inayoitwa BitLord Hapa  na uiweke ndani ya kompyuta yako (install).

3. Ukishaweka hiyo programu kwenye kompyuta yako, ifungue.

4. Baada ya  kufunguka, utaona sehemu ya kutafuta. Andika jina la filamu unayoitaka halafu ubonyeze tafuta.

5. Itakuja orodha ya majina ya filamu yanayofanana na uliloandika.

6. Chagua na ubonyeze kiunganishi cha filamu unachokipenda cha kupakua chenye alama ya mshale unaoelekea chini.

7. Ukurasa mdogo utafunguka, chagua kiunganishi kilichoandikwa pakua.

8. Baada ya hapo programu itaanza kupakua filamu iliyochaguliwa.

9. Iache ipakue na uendelee na matumizi yako ya kompyuta kama kawaida.

10. Furahia kupakua filamu mpya kila siku!

Kama taarifa hii imekusaidia, tafadhari like page yetu au tupia ‘comments’ au sambaza ukurasa huu!

Comments

comments