Chezea Wanawake Wewe!!!

simu

Jamaa mmoja alibahatika kuoa mke mzuri sana toka mkoa fulani hivi hapa Tanzania. Baada ya mwaka mmoja wa ndoa yule mwanamke akaanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na ‘Kiserengeti’ kimojawapo katika mtaa wao! Siku moja usiku mtu na mke wake walikuwa wamekaa chumbani na ghafla ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu ya yule mwanamke.

Katika hali ya kushangaza yule mwanamke akaanza kulia baada ya kupokea ujumbe kutoka kwa Kiserengeti chake kikimwambia mapenzi yao yamefikia kikomo. Mume ikabidi amwulize mkewe na mazungumzo yao yalikuwa hivi,


Mume: Nani kakutumia sms sasa hivi?

Mke: Dada!

Mume: Inasemaje?

Mke: Ananielekeza jinsi ya kupika pilau!

Mume: Sasa mbona unalia?

Mke: Si nimefika sehemu ya kukata vitunguu!

**********


Comments

comments