Chezea Safari Ya Mbinguni Wewe!

safari ya mbinguni

Jamaa mmoja akiwa na mtutu wa kivita maarufu kama AK47 alivamia kanisa moja la kiroho na kukuta watu wanafanya ibada. Akiwa ameuelekeza mtutu wake juu jamaa alianza kupaza sauti huku akielekea madhabahuni.

“Nani ni mtoto wa mungu hapa?” Jamaa alihoji kwa ubabe. “Nauliza hivi, nani ni mtoto wa mungu hapa ili nimpeleke sasa hivi kwa baba yake mbinguni!”

Waumini wote walikaa kimya na jamaa akaongeza mkwara kwa kufyatua risasi tatu kwenye paa la kanisa. Waumini wote wakapaza sauti, “ni mchungaji. Kila siku huwa anasema yeye ni mtoto wa mungu.”

Kwa upole na unyenyekevu mwingi mchungaji akajibu, “mbona mnanisaliti wapendwa? Nyote nyie mnajua kwamba mimi ni mtoto wa Githinji. Sasa ninahusianaje na huyo mungu!”

Chezea safari ya mbinguni wewe!!!

Comments

comments