Mkandarasi

Chezea Mkandarasi!!!! Juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa ikulu ya Magogoni ulianguka. Ikulu ikatangaza uhitaji wa kujenga ukuta ule wakapelekwa wakandarasi watatu ili kupitia mchakato wa uteuzi wa atakayeshinda zabuni hiyo ya ujenzi kwa bei nafuu na uimara mkubwa!

Wa kwanza alikuwa MUHINDI, wapili alikuwa MCHINA na wa tatu alikuwa MBONGO!

MUHINDI: Nitajenga kwa milioni 90, milioni 40 vifaa, 40 nyingine mafundi na 10 faida yangu.


MCHINA: Nitajenga kwa milioni 70, milioni 30 vifaa, 30 nyingine za mafundi na 10 itakuwa faida yangu.

MBONGO: Mimi nitajenga kwa milioni 270!

MSIMAMIZI WA MAGOGONI: Wewe wa kupima sio bure una wazimu, yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja bei ya chini kabisa!

MBONGO: Milioni 100 zako, 100 zangu halafu zile 70 tunaajiri huyu MCHINA!

MSIMAMIZI WA MAGOGONI: Heee! Eti! Ehee!

MBONGO: Changamkia fursa!

**********


Comments

comments