bwege

Mdada mmoja mrembo sana alikuwa kapewa talaka na mumewe akahamia nyumba aliyokuwa kapanga DEVI.

DEVI alipomuona mpangaji mpya roho yote ikamtoka. Akajitahidi kila njia kumuonyesha kuwa naye yupo na ni bachela, mdada akawa anaendelea na shughuli zake bila hata kuonyesha dalili za kumwona DEVI.

Jioni moja DEVI akiwa kapumzika akasikia hodi kwenye chumba chake, alipofungua akakutana uso kwa uso na mdada mpangaji, kapendeza sana na akiwa kavaa kimini cha nguvu;

MDADA: Samahani kaka Devi, yaani nimekaa muda mrefu mpweke nimeona leo lazima nitoke nikajirushe kidogo kisha nipate bwana niondoe uchovu. Vipi we uko free?

DEVI: Mimi sana tu niko free sina kitu chochote ninachofanya jioni hii, yaani niko free kabisa si unaona mwenyewe niko free sina ishu kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

MDADA: Loh nakushukuru sana kaka yangu, basi ngoja nikuletee watoto wangu ushinde nao mpaka nitakaporudi.

Bora Kukamua Maziwa Kuliko Kushika Pembe

Comments

comments